Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bi. Nteghenjwa Hosseah akiwa katika kikao maalum na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini kutoka kwenye Sekretarieti za Mikoa, kilichofanyika mjini Morogoro katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA).
Kikao hicho kina lengo la kukumbushana na kuhimiza uwajibikaji wa Maafisa Habari wa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa mwaka 2025.