Naibu waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Doto Biteko akizungumza na Mawaziri wa Nishati, Viongozi na wadau mbalimbali waliohudhuria mkutano wa mawaziri wa Nishati na mawaziri wa Fedha wa nchi za Afrika pamoja na wadau wa maendeleo kuhusu Nishati ulioanza leo kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere JNICC jijini Dar es salaam leo Januari 27, 2025.
……………..
Leo, Januari 27, 2025, mkutano muhimu wa nishati unaowakutanisha Mawaziri wa Nishati, Mawaziri wa Fedha, na wadau wa maendeleo unafanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Mkutano huu, unaojulikana kama “Mission 300”, unalenga kujadili mikakati ya kuhakikisha upatikanaji wa nishati kwa watu milioni 300 barani Afrika. Viongozi mbalimbali, wakiwemo Wakuu wa Nchi za Afrika, wanahudhuria mkutano huu.
Mawaziri wa Nishati 60 wanashiriki katika mkutano huo ambao umefunguliwa na Naibu Waziri Mkuu wa Tanzania na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko.