Na Farida Mangube
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa kushirikiana na Shirika la Misaada la Watu wa Japan, Japan International Cooperation Agency (JICA), wamekubaliana kushirikiana kukuza ujuzi katika sekta ya kilimo na umwagiliaji kupitia mafunzo na uzoefu kutoka kwa wataalam mbalimbali.
Akizungumza baada ya kupokea ujumbe wa wageni kutoka JICA, ulioongozwa na Mwakilishi Mkuu wa JICA Tanzania, Ndg. ARA Hitoshi, Profesa Samuel Kabote (kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma) alisema ushirikiano huo unalenga kuhamasisha maendeleo endelevu nchini kwa kutumia uzoefu wa Japan katika kilimo na teknolojia ya umwagiliaji.
Profesa Kabote alieleza kuwa historia ya Japan, ambayo haijawahi kutawaliwa na nchi za kikoloni, ni ya kipekee, na maendeleo yake makubwa katika sekta ya kilimo ni mfano wa kuigwa. Ujuzi huo utatolewa kwa wanafunzi wa SUA kupitia mikutano maalum itakayowaleta pamoja wataalam wa Japan na Tanzania.
“Mkutano wa kwanza unatarajiwa kufanyika SUA tarehe 18 Februari, na lengo ni kuwahamasisha wanafunzi kushirikiana na kujifunza hatua ambazo Japan ilichukua kufanikisha maendeleo yake katika kilimo. Hii itawasaidia wanafunzi si tu kitaaluma bali pia kuchangia maendeleo ya nchi yao,” alisema Profesa Kabote.
Kwa upande wake, Afisa Mradi wa JICA CHAIR, Ndugu Alfred Zakaria, alisema ujio wa sasa wa JICA unahusiana na maandalizi ya kika