Kivuko cha Mv.Bukondo ambacho kitafanya safari zake Bwiro Bukondo katika Wilaya ya Ukerewe Mkoani Mwanza
………………..
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Vivuko vitano vinavyo jengwa kwenye Karakana ya Songoro Marine vitakapokamilika vitawasaidia wananchi wa Wilaya za,Magu,Misungwi,Sengerema na Ukerewe katika shughuli zao za kiuchumi na kijamii.
Hayo yamebainishwa Leo Januari 24, 2025 na Waziri wa Uvuvi Mh. Abdallah Ulega wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi wa vivuko vitano vinavyojengwa kwenye Karakana ya Songoro Marine Jijini Mwanza.
Amesema vivuko hivyo vitakuwa mkombozi kwa wananchi wa maeneo hayo kwenye masuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo kwenda kwenye huduma za afya.
“Leo nimeshuhudia vivuko hivi vyenye uwezo wa kubeba tani 100 za mizigo na abiria 200 hii ni hatua kubwa sana kwa nchi yetu kwani haijawahi kutokea tangu tupate uhuru”, amesema Waziri Ulega
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Songoro Marine, Meja Songoro ambae ni mkandarasi mzawa anaetengeneza vivuko hivyo amesema vivuko hivyo viko kwenye hatua za mwisho za ukamilishaji ili viweze kuanza kazi
Akizungumzia kivuko cha Bwiro Bukondo Songoro amesema ujenzi wake umefikia asilimia 91.3 na kitakapokamilika kitakuwa na uwezo wa kubeba abiria 200 na tani 100 za mizigo.
“Tunatarajia kukiingiza kwenye maji Januari 31 mwaka huu kwaajili ya kukamilisha ujenzi na kukifanyia majaribio ili itakapofika machi 31, 2025 kiwe kimekamilika”, amesema Ulega.