Kamishna Mkuu wa TRA, Bw. Yusuf Mwenda, akikabidhi tuzo hiyo kwa Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Moureen Mwaimale, kwa niaba ya Kamishna wa Uhifadhi TANAPA .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza nanwageni waalikwa katika hafla hiyo.
…………….
Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limeibuka kidedea kwa kutunukiwa tuzo ya juu zaidi katika kipengele cha taasisi zilizochangia kufanikisha na kurahisisha ukusanyaji wa kodi kwa ngazi ya taifa. Tuzo hiyo imetolewa katika hafla ya utoaji tuzo za walipakodi bora kwa mwaka 2023/2024, iliyofanyika leo Alhamisi, Januari 23, 2025, katika ukumbi wa Super Dome, Masaki, jijini Dar es Salaam.
Hafla hiyo, iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ilihudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye alikuwepo kushuhudia tukio hilo muhimu pamoja na viongozi waandamizi wa serikali na sekta binafsi,
Tuzo hiyo ya heshima ilikabidhiwa na Kamishna Mkuu wa TRA, Bw. Yusuf Mwenda, na kupokelewa kwa niaba ya Kamishna wa Uhifadhi TANAPA na Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Moureen Mwaimale, anayesimamia idara ya fedha TANAPA Makao Makuu.
Akizungumza baada ya hafla hiyo, TANAPA ilieleza kujivunia mchango wake katika kuhakikisha uwajibikaji wa kodi na kuchangia maendeleo ya taifa, huku ikiahidi kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kusaidia juhudi za serikali za kuongeza mapato ya ndani.