ufanisi kwa mwaka 2025, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. Hamza Johari, akizungumza katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika lililofanyika katika chuo Uongozi cha Mwalimu Nyerere (Mwalimu Julius Nyerere Leadership School) Kibaha mkoani Pwani leo Januari 24, 2025.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Bw. Eliakim Maswi, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo akizungumza na Baraza hilo lililofanyika chuo Uongozi cha Mwalimu Nyerere (Mwalimu Julius Nyerere Leadership School) Kibaha mkoani Pwani leo Januari 24, 2025.
Mhe. Samwel M. Maneno, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali akimkaribisha mgeni rasmi katika kikao cha Baraza hilo ili kuzungumza na wajumbe mbalimbali wa Baraza waliohudhuria.
…………….
Na John Bukuku, Kibaha Pwani
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imefanikiwa kupiga hatua kubwa katika utekelezaji wa majukumu yake kwa kipindi cha Julai hadi Desemba 2024, ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo kwa wanasheria, jambo lililosaidia kuongeza uwezo wa kisheria wa kushughulikia changamoto na kupunguza kero za wananchi.
Akizungumza leo, Januari 24, 2025, jijini Dar es Salaam katika Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo, lililofanyika katika chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere (Mwalimu Julius Nyerere Leadership School) Kibaha mkoani Pwani leo Januari 24, 2025 ambacho kilikuwa na lengo la kutathmini utendaji kazi wa mwaka 2024 na kuweka mikakati ya kuboresha ufanisi kwa mwaka 2025, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. Hamza Johari, alisema mafanikio makubwa yamepatikana katika mwaka uliopita.
Bw. Johari alisema kuwa moja ya mafanikio makubwa ni kuanzishwa kwa kliniki ya sheria inayotekelezwa nchi nzima, kwa lengo la kusogeza huduma za kisheria karibu zaidi na wananchi.
“Kwa sasa, kliniki ya sheria inaendelea mkoani Kilimanjaro, na tumeshuhudia idadi kubwa ya wananchi wakifika kupata huduma mbalimbali za kisheria. Tunaamini jitihada hizi zitapunguza changamoto na kero walizokuwa nazo wananchi,” alisema Bw. Johari.
Aidha, aliongeza kuwa ofisi hiyo imefanikiwa kupitia na kuhakiki mikataba ya taasisi mbalimbali kwa lengo la kutoa ushauri wa kisheria, huku akisisitiza umuhimu wa kuendelea kuboresha mafunzo kwa watumishi.
Awali, Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Bw. Eliakim Maswi, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo, aliwataka wafanyakazi wa ofisi hiyo kuwa huru kutoa maoni na ushauri katika baraza hilo ili kuimarisha utendaji kazi.
Bw. Maswi alisisitiza umuhimu wa kuboresha mifumo ya TEHAMA katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na kuimarisha ushirikiano wa ndani na nje ya ofisi ili kuongeza tija.
“Wizara ya Katiba na Sheria itaendelea kushirikiana na viongozi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhakikisha changamoto zote zinazowasilishwa zinatafutiwa ufumbuzi,” alisema Bw. Maswi.
Aidha, Katibu Mkuu Maswi alitoa wito kwa wafanyakazi wa ofisi hiyo kuzingatia sheria na miongozo kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu, ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani, umoja, upendo, na mshikamano.