Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura, Januari 24,2025 amekutana na kuzungumza na Maafisa, Wakaguzi na Askari wa vyeo mbalimbali kutoka Kanda Maalum Dar es salaam ambao wataimarisha usalama kwenye mkutano utakaowakutanisha zaidi ya Marais 51 na Mawaziri wa Fedha na Nishati 60 wa Afrika watakaoshiriki Mkutano wa Nishati utakaofanyika Jijini Dar es Salaam Januari 27 hadi 28, mwaka huu 2025. Picha na Jeshi la Polisi