Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akigonga kengele kuashiria kuorodhoreshwa rasmi kwa Hati Fungani ya Benki ya Azania ijulikanayo kama Bondi Yangu, katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Hafla iliyofanyika katika Ofisi za DSE, jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine aliziasa taasisi zingine kuiga mfano wa Azania Bank wa kujiorodhesha kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam na kutoa fursa kwa wananchi kushiriki kukuza uchumi wao binafsi na uchumi wa nchi kwa njia za kidijitali. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dar es Salaam)