MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akifungwa kiskafu na Vijana wa UVCCM, baada ya kuwasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar, akitokea Dodoma katika Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM uliyofanyika wiki iliyopita na kuchaguliwa kugombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar mwaka 2025.(Picha na Ikulu)
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakiweka shada la maua katika kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh. Abeid Amani Karume, na kuzungumza na Wazee wa CCM Zanzibar katika ukumbi wa Afisi Kuu Kisiwandui Wilaya ya Mjini Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu).
VIONGOZI wa Serikali, Chama na Wananchi mbalimbali wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayipo pichani) akizungumza na wananchi katika viwanja vya Mapinduzi Square Michezani, wakati wa hafla ya mapokezi akitokea Dodoma katika Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM, uliyofanyika wiki ilipita.(Picha na Ikulu)
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambaev pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Wananchi katika viwanja vya Mapinduzi Square Michezaji Kisonge Wilaya ya Mjini Unguja, katika hafla ya mapokezi yake akitokea Dodoma katika Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM uliyofanyika wiki iliyopita na kuchaguliwa kugombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar mwaka 2025.(Picha na Ikulu)