MAKAMU Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi IPCC DK. Ladislaus Chang’a amesema joto limeongezeka kwa nyuzi 1.55 mwaka 2024 ikiwani rekodi ya juu kuwahi kurekodiwa Diniani.
Akizungumza katika warsha ya wanahabari kuhusu Utabiri wa Mvua za Msimu wa Masika Januari 22, 2025, Dk. Chang’a amesema ongezeko hilo ni la dunia huku kwa Tanzania joto likiongezeka kwa 0.7
Amesema juhudi za makusudi zinapaswa kuchukuliwa ili kunusuru madhara yanayoweza kutokea ikiwemo ongezeko la vimbunga.
Amesema juhudi zaidi zinatakiwa katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani kote ili kupunguza ongezeko hilo la joto.
Kwa upande wa miundombinu, Kaimu Mkurugenzi huyo ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kuwekeza kwenye sekta ya hali ya hewa katika miundombinu na rasilimali watu.