Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Newtan Insurance Bw. Nelson Rwihula akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 20, 2025 jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa ya kubadilisha jina la kampuni kutoka jina la UAP Insurance Tanzania na kuwa Newtan Insurance
Mwenyekiti wa Bodi Kampuni ya Newtan Insurance Bw. Moses Obonyo akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 20, 2025 jijini Dar es Salaam wakati wakitoa taarifa ya kubadilisha jina la kampuni kutoka jina la UAP Insurance Tanzania na kuwa Newtan Insurance.
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Oldmutual Afrika Mashariki Arthur Oginga (wa kwanza kushoto) akipokea ufunguo wa Newtan Insurance kutoka wa Mwenyekii wa Bw. Moses Obonyo, katikati ni mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Newtan Insurance Bw. Nelson Rwihula.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Newtan Insurance wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari
……….
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Kampuni ya Newtan Insurance imejipanga kuendelea kutoa huduma bora kwa jamii ikiwemo elimu kuhusu umuhimu wa bima, huku wakieleza kuwa sasa wamebadilisha jina la UAP Insurance Tanzania kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kubadilika kwa wana hisa katika kampuni hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 20, 2025 jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Newtan Insurance Bw. Nelson Rwihula, amesema kuwa wamebadilisha jina la Kampuni kutoka jina la UAP Insurance Tanzania na kuwa Newtan Insurance, huku akiwatoa hofu wateja na wadau mbalimbali kuwa hakuna mabadiliko yoyote huduma kulingana na makuliano walioingia na wateja kuhusu kutoa huduma ya bima.
Bw. Rwihula amesema kuwa mabadiliko ya jina hayataathiri mikataba ya wateja wao wa sasa na wanaokuja, huku akifafanua kuwa wataendelea kuwajibika kutoa huduma ya bima.
“Tutaendelea kuwajibika kwa wateja wetu pale wanapopata na majanga, mabadiliko ya jina hayatapunguza malengo katika utekelezaji wa majukumu yetu kulingana na makubaliano na wateja, tutatoa ushirikiano wakati wote katika masuala ya bima” amesema Bw. Rwihula.
Amesema kuwa wanaendelea kuongeza wigo katika kutoa huduma za bima ikiwemo bima ya kilimo , huku akieleza kuwa mwaka wa 2024 walifanikiwa kuwalipa fidia wakulima wadogo 1, 200 waliopata majanga ya mazao.
Bw. Rwihula amesema kuwa wamekuwa na utaratibu wa kuwafikia wakulima ambao hawafikiwi na huduma ya bima na kuwapatia huduma hiyo muhimu.
Kampuni ya Newtan Insurance wameanza kutoa huduma ya bima nchini mwaka mwaka 2009 na kukijikita kutoa bima ya mali na majanga, mwaka 2024 wamefanikiwa kutoa fidia kwa wakulima wa tumbaku zaidi ya bilioni moja ili kufidia majanga waliopata katika zao hilo.