Mkuu wa Mkoa Tanga Balozi Dkt Batilda Burian amempongeza Rais Dkt Samia Suluhu kwa kazi kubwa ya maendeleo anayoifanya nchini ikiwemo mkoani humo na hivyo kusaidia kufungua fursa za kiuchumi kwenye mkoa huo
Balozi Dkt Batilda ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasilishwa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi ( CCM) upande wa Zanzibar na Tanzania bara katika mkutano mkuu maalumu wa ccm uliofanyika mjini Dodoma.
Balozi Dkt Batilda amesema wanatanga wanashuhudia utendaji mkubwa katika huduma mbalimbali ikiwemo za kijamii na hata katika miundombinu, lakini pia masuala ya mazima ya uchumi namna ulivyokuwa na mtazamo mzima wa upanuzi wa bandari na mambo mengine makubwa yameweza kufanyika.
“Leo pale Tanga ukifika utakutana na uwekezaji mkubwa wa bomba la mafuta ambalo litasafirisha Mafuta ghafi kutoka hoima nchini Uganda hadi Chongeleani Jijini Tanga ambao utaufungua mkoa wetu kiuchumi na kuinua pato la Mkoa na Taifa Kwa ujumla na mradi huu ni muhimu kwa Maendeleo”Alisema.