Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu NBC Tanzania Bara Yanga SC imeishia hatua ya 16 bora ya mashindano ya Klabu Bigwa Afrika baada kushika nafasi ya tatu kwenye kundi A kufatia sare ya bila kufungana na MC Alger katika mchezo uliopigwa leo Januaria 18, 2025 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Yanga SC ilihitaji ushindi ili kufuzu kwa mara pili mfululizo hatua ya robo fainali lakini mipango ya MC Alger ilifanikiwa kuwalazimisha sare.
Katika mchezo mwenyengine wa kundi A Tp Mazembe wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4- 0 dhidi ya Al Hilali Omdurman katika mchezo uliopigwa jijini Lubumbashi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Kufatia matokeo hayo Al Hilali Omdurman na MC Alger wamefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Klabu Bigwa Barani Africa.