Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Dkt. Zakia Mohamed Abubakar akizungumza hii leo Januari 18, 2025 wakati akifunga mafunzo ya siku mbili kwa watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ngazi ya mkoa, mkoani Mtwara ambapo amewahimiza watendaji hao kuhakikisha wanahamasisha wananchi wenye sifa ili wajitokeze kujiandikisha na kupata haki yao ya kikatiba itakayowawezesha kushiriki katika kuchagua viongozi wao.
la Wapiga Kura katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma wametakiwa kutekeleza
majukumu yao kwa kuzingatia sheria, kanuni, maelekezo na miongozo itakayotolewa
na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.
pia ni Jaji wa Mahakama Kuu, Mhe. Asina Omar leo tarehe 18 Januari, 2025 wakati
akifunga mafunzo ya watendaji wa uboreshaji wa Daftari ngazi ya mkoa, Mkoani Lindi
ikiwa ni maandalizi ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
kuzingatia sheria, kanuni, maelekezo na miongozo itakayotolewa na Tume,”
amesema Jaji Asina.
umuhimu wa zoezi la uboreshaji wa Daftari na kwamba elimu na ujuzi walioupata
vitawasaidia kutekeleza kwa nadharia na vitendo yale yote waliyofundishwa.
hili la kitaifa na kwamba baada ya ninyi kufundishwa na kuelekezwa ipasavyo
katika mafunzo haya, elimu na ujuzi mliopata vitawasaidia kutekeleza kwa
nadharia na vitendo yale yote mliyofundishwa,” amesema.
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe.
Dkt. Zakia Mohamed Abubakar amewahimiza watendaji hao kuhakikisha wanahamasisha
wananchi wenye sifa ili wajitokeze kujiandikisha na kupata haki yao ya kikatiba
itakayowawezesha kushiriki katika kuchagua viongozi wao.
zoezi hili kukamilika watu watakaokuwa wamepatiwa kadi watakuwa ni wapiga kura
halali.
la uhamasishaji linawahusu moja kwa moja ninyi watendaji, kwa kushirikiana na
wadau wengine katika maeneo yenu kupitia nyenzo mlizo nazo,” amesema Mhe. Zakia.
Mjumbe wa Tume, Mhe. Magdalena Rwebangira ambaye aliwakumbusha watendaji hao
kuwa makini katika kila eneo la usambazaji na utunzaji wa vifaa, mafunzo yote
na muda sahihi wa ufunguaji na ufungaji wa vituo vya kuandikishia wapiga kura.
Mafunzo hayo yamefanyika
ikiwa ni maandalizi ya uboreshaji wa Daftari mkoani Mtwara, Lindi na mkoa wa Ruvuma
kwenye Halmashauri za Wilaya ya Madaba, Namtumbo na Tunduri ambapo uboreshaji utafanyika kwa siku saba
kuanzia tarehe 28 Januari, 2025 hadi tarehe 03 Februari, 2025 na vituo
vitafunguliwa saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.