Mwanasiasa mkongwe Stephen Wasira, ambaye amewahi kushika nyadhifa mbalimbali ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikalini, ameteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara.
Wasira amepewa nafasi hiyo kufuatia ombi la kustaafu kwa Abdulrahman Kinana, aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, aliyeamua kuachia wadhifa huo mwaka 2024 baada ya kuhudumu kwa muda mrefu ndani ya chama.
Teuzi ya Wasira itathibitishwa rasmi baada ya kupigiwa kura na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, ambapo jumla ya wajumbe 1,924 wanashiriki mkutano huo leo, Januari 18, 2024.
Wasira ni miongoni mwa wanasiasa waliotoa mchango mkubwa katika uongozi wa chama na taifa kwa ujumla, hivyo kuteuliwa kwake kunaleta matumaini mapya kwa wanachama wa CCM.