Msimamizi wa mradi wa maji wa miji 28 kutoka Mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Manispaa ya Songea(Souwasa)Mhandisi Vicent Bahemana kulia,akionyesha mchoro wa mradi huo kwa wajumbe wa kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi wilaya ya Songea wakiongozwa na Mwenyekiti wake Mwinyi Msolomi aliyevaa kaunda suti wakati wa ziara ya wajumbe hao walipotembelea mradi huo jana.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Songea mjini mkoani Ruvuma Mwinyi Msolomi katikati na katibu wa Chama hicho James Mgego kushoto, wakikagua tenki la kuhifadhi maji lita milioni 2 eneo la Chandamali linalojengwa kupitia mradi wa maji wa miji 28 katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma,kulia msimamizi wa mradi huo kutoka Mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Songea(Souwasa) Mhandisi Vicent Bahemana.
Msimamizi wa mradi wa maji wa miji 28 unaotekelezwa katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma kwa gharama ya Sh.bilioni 145.77 Mhandisi Vicent Bahemana,akitoa ufafanuzi kwa wajumbe wa kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi wilaya ya Songea mjini, kuhusu maendelea ya ujenzi wa mradi huo baada ya wajumbe hao kufika eneo la Mahiro ambako kunatarajia kujengwa tenki kubwa la kuhifadhi lita milioni 5 za maji.