Mwenyekiti wa tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufani, Mhe. Jacobs Mwambegele akifungua mafunzo ya siku
Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na
Maafisa TEHAMA wa halmashauri yaliyoanza leo tarehe 17 hadi 18 Januari, 2025
Mkoani Mtwara ambapo amewataka watendaji hao kuhakikisha wanatunza vifaa vya
uandikishaji ili viweze kutumika katika maeneo mengine nchini pamoja na kuzangitia
mafunzo hayo ili wakafanikishe zoezi hilo muhimu.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya uchaguzi, Ndg. Kailima, R. K akizungumza jambo wakati wa mafunzo hayo.
wa Mtwara, Fredrick Mwanamboje akiwasilisha mada ya uraia kwa watendaji wa
uboreshaji mkoa wa Mtwara wakati wa mafunzo ya siku mbili ya watendaji hao
ikiwa ni maandalizi ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura mkoani huo.
Watendaji hao ni pamoja na Mratibu wa Uandikishaji wa Mkoa, Maafisa
Waandikishaji, Maafisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa
Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri.
Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa (Mst) Mbarouk Salim Mbarouk leo tarehe 17 Januari, 2025 amefungua mafunzo ya watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ngazi ya mkoa, mkoani Lindi ambapo amewataka watendaji hao kutunza vifaa vya uboreshaji wa Daftari na kuzingatia sheria, kanuni na maelekezo ya Tume wakati wote wa utendaji wao.
Mafunzo
kwa Watendaji wa uchaguzi katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma katika
halmashauri za wilaya ya Madaba, Namtumbo na Tunduru ikiwa ni mzunguko wa 10 wa
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura yamefunguliwa leo mkoani Mtwara na
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe.
Jacobs Mwambegele.
Mafunzo
kama hayo pia yamefunguliwa katika mikoa ya Lindi na Ruvuma ambapo mkoani Lindi
mafunzo hayo yamefunguliwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume, Jaji wa Rufani (Mstaafu)
Mhe. Mbarouk Salim Mbarouk na mkoani Ruvuma, mafunzo hayo yamefunguliwa na
Mjumbe wa Tume Mhe. Magdalena Rwebangira.
Akifungua
mafunzo ya siku mbili kwa Waratibu wa Uandikishaji wa mkoa, Maafisa
Waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa
Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa halmashauri yaliyoanza leo tarehe
17 hadi 18 Januari, 2025 Mkoani Mtwara Mhe. Jaji Mwambegele amewataka watendaji
hao kuhakikisha wanatunza
vifaa vya uandikishaji ili viweze kutumika katika maeneo mengine nchini.
Amesema
ni muhimu kutekeleza majukumu yenu kwa umakini katika kila eneo ikiwemo utunzaji
wa vifaa vya uandikishaji hasa ikizingatiwa kuwa, vifaa hivi vimenunuliwa kwa
gharama kubwa sana na vinatarajiwa kutumika katika maeneo mengine ya
uandikishaji nchini.
Mkoani
Lindi, Makamu Mwenyekiti wa Tume Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani Mstaafu
Mbarouk Salim Mbarouk amewaambia watendaji hao kuwa wakati wa uboreshaji wa Daftari katika mikoa hiyo, mawakala wa vyama vya siasa
wataruhusiwa kuwepo katika vituo vya kuandikisha wapiga kura jambo ambalo
litasaidia kuleta uwazi katika zoezi zima lakini pia mawakala hao watasaidia
kutambua waombaji wa eneo husika hivyo kupunguza kutokea kwa vurugu zisizokuwa
za lazima.
Amewaambia
watendaji hao kuwa wakati wa uboreshaji wa Daftari mawakala wa vyama vya siasa
wataruhusiwa kuwepo katika vituo vya kuandikisha wapiga kura jambo ambalo
litasaidia kuleta uwazi katika zoezi zima lakini pia mawakala hao watasaidia
kutambua waombaji wa eneo husika hivyo kupunguza kutokea kwa vurugu zisizokuwa
za lazima.
Hata
hivyo Mhe. Jaji Mbarouk amesisitiza kuwa mawakala hao hawaruhusiwi kuwaingilia watendaji
wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.
Naye
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Magdalena Rwebangira ambaye
amefungua mafunzo hayo kwa watendaji wa uboreshaji katika mkoa wa Ruvuma ameeleza
kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea umahiri watendaji hao ili waweze
kuwafundisha Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Kata kisha nao watatoa
mafunzo hayo kwa Waendeshaji wa Vifaa vya Bayometriki na Waandishi Wasaidizi
ambao ndio watakaohusika na uandikishaji wa wapiga kura vituoni.
Ameongeza
kuwa Maafisa TEHAMA nao watapatiwa mafunzo maalum ya jinsi ya kukabiliana na
changamoto mbalimbali za kiufundi (Troubleshooting) endapo zitajitokeza wakati
wa zoezi la uandikishaji wa wapiga kura vituoni.
Mafunzo
hayo ambayo yanafanyika kwa muda wa siku mbili ni sehemu ya maandalizi ya
uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika mikoa ya Mtwara, Lindi na
Ruvuma katika halmashauri za wilaya ya Madaba, Namtumbo na Tunduru ambao
utafanyika kuanzia tarehe 28 Januari, 2025 hadi tarehe 03 Februari, 2025.