Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis
Hamza Khamis Januari 16, 2025 jijini Dodoma akifafanua jambo kwa Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira, wakati akiwasilisha taarifa ya
utekelezaji wa maazimio ya Bunge yaliyotokana na taarifa ya mwaka ya
shughuli za Kamati iliyowasilishwa bungeni Februari, 2024.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira Mhe.
Jackson Kiswaga akiongoza kikao cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa
maazimio ya Bunge yaliyotokana na taarifa ya mwaka ya shughuli za Kamati
iliyowasilishwa bungeni Februari, 2024, kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais leo
Januari 16, 2025 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja akifafanua
jambo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira, wakati wa
kikao cha kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya Bunge
yaliyotokana na taarifa ya mwaka ya shughuli za Kamati iliyowasilishwa
bungeni Februari, 2024.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira wakifuatilia
kikao cha kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya Bunge
yaliyotokana na taarifa ya mwaka ya shughuli za Kamati iliyowasilishwa
bungeni Februari, 2024, kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais leo Januari 16, 2025
jijini Dodoma.
…………..
Serikali inaendelea na ukamilishaji wa taratibu za kuanzisha Mfuko wa Nishati
safi ya kupikia ili kuweka ruzuku itakayowawezesha wananchi wa kipato cha
chini kumudu bei ya gesi.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis
Hamza Khamis ameiarifu Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira
leo Januari 16, 2025 jijini Dodoma, alipowasilisha taarifa ya utekelezaji wa
maazimio ya Bunge yaliyotokana na taarifa ya mwaka ya shughuli za Kamati
iliyowasilishwa bungeni Februari, 2024.
Amesema Kanuni za Usimamizi wa miradi ya biashara ya kaboni zimebainisha
ruzuku kupitia hakimiliki za kaboni zinazopatikana kutokana na kupunguza
matumizi ya nishati inayochafua mazingira, hivyo ruzuku hii ni sehemu ya
juhudi za kitaifa za kutekeleza malengo ya kupunguza gharama kwa watumiji
wa nishati safi.
Mhe. Khamisi ameileza kamati hiyo kuwa katika jitihada za kupunguza
gharama za matumizi ya nishati mbadala, Serikali imesaini makubaliano ya
awali na wawekezaji kuhusu ruzuku ya shilingi bilioni 8.64 kwenye nishati safi
ya kupikia mbapo jumla ya majiko 452,455 yamepata ruzuku.
Aidha, Naibu Waziri Khamis amesema Serikali inaendelea kuhamasisha
matumizi ya nishati mbadala kwa njia mbalimbali ikiwemo utoaji wa elimu kwa
umma kupitia vyombo vya habari, ziara za viongozi.
Kwa upande mwingine amesema kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais inaendelea
kushirikiana na wadau wengine wakiwemo Ofisi ya Rais-TAMISEMI na Wakala
wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa lengo la kuhamasisha na kuhimiza
Halmashauri zote za vijiji kuainisha misitu yote ya vijiji yenye sifa ya
kuingizwa kwenye mpango wa Biashara ya Kaboni.
Amefafanua kuwa uhamasishaji wa jamii kuhusu umuhimu wa biashara ya
kaboni katika kuhifadhi mazingira na kuongeza kipato kwa jamii unaendelea
kutolewa kwa wananchi ambapo Serikali inaendelea kusimamia na
kuhakikisha kuwa mikataba ya biashara ya kaboni inanufaisha wananchi na
inafanyika kwa mujibu wa Kanuni za usimamizi wa biashara ya kaboni.
Kwa upande wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira
inayoongozwa na Mwenyekiti Mhe. Jackson Kiswaga imeipongeza Ofisi ya
Makamu wa Rais kwa kuwakutanisha wadau na kujadili changamoto za
mazingira ili kuzipatia ufumbuzi.
Pamoja na hayo imesisitiza elimu ya mazingira iendelee kutolewa ili wananchi
waweze kupata uelewa na kuachana na vitendo vya uharibifu wa mazingira
vikiwemo uchomaji na ukataji wa miti.
Pia, imesema elimu ya nishati safi ipewe msukumo kwani wananchi wengi
hususan wa maeneo ya vijijini hawana uelewa wa umuhimu wa matumizi ya
nishati safi ya kupikia hivyo kwa kuwapa elimu wataachana na matumizi ya
kuni na mkaa.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja akifafanua
hoja amesema hadi kufikia Desemba 30, 2024, maombi ya miradi 65 ya
biashara ya kaboni yamepokelewa.
Amefafanua kuwa jumla ya miradi sita imepata barua za kukubaliwa kuanza
mchakato wakati miradi sita imetimiza vigezo na hatua za kupatiwa barua
inaendelea.