WACHEZAJI wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes wakiwa na Kocha Mkuu wa Timu hiyo Hemed Moroco (kushoto) wakishangilia wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia wakati wa hafla ya Chakula Maalumu alichowaandaliwa katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar leo 15-1-2025, kwa ajili ya kuwapongeza kwa kutowa Kombe la Mapinduzi kwa mwaka 2025, katika mchezo wa fainali na kuifunga Timu ya Taifa ya Bukinafaso, mchezo uliofanyika Uwanja wa Gombani Chakechake Pemba 13-1-2025, kwa ushindi wa bao 2-1.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar, katika hafla ya kuwapongeza Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes kwa kutowa Ubingwa wa Kombe la Mapinduzi Cup 2025, kwa kuifunga Timu ya Taifa ya Burkina Faso katika mchezo wa Fainali uliyofanyika katika uwanja wa Gombani Chakechake Pemba 13-1-2025, wakati wa hafla ya chakula maalumu alichowaandalia katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar leo 15-1-2025.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi, akimkabidhi fedha tasilimu shilingi milioni 50 Nahodha wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes Feisal Salum (Feitoto) wakati wa hafla ya kuipongeza Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes kwa kutowa Kombe la Mapinduzi Cup 2025, katika mchezo wa fainali na Timu ya Taifa ya Burkina Faso, uliyofanyika katika uwanja wa Gombani Chakechake Pemba 13-1-2025 na kuibuka kwa ushindi wa bao 2-1, wakati wa hafla ya chakula maalumu alichowaandalia katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar leo.15-1-2025.(Picha na Ikulu).
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhi zawadi ya Shilingi Milioni 50 kwa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes kwa kutowa Ubingwa wa Kombe la Mapinduzi Cup 2025 ,kwa kuifunga Timu ya Taifa ya Burkina Faso,katika mchezo wa Fainali uliofanyika katika uwanja wa Gombani Chakechake Pemba 13-1-2025, na kuibuka kwa mshindi wa bao 2-1, akimkabidhi Nahodha wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes Feisal Salum (Feitoto) na (kulia kwake) Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe.Tabia Maulid Mwita.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi akikabidhiwa Kombe la Ubingwa wa Michuano ya Mapinduzi Cup 2025, na Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes Hemed Moroco, wakati wa hafla ya kuipongeza Timu hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar na kujumuika na Wachezaji hao katika dhifa ya chakula maalumu alichowandalia leo 15-1-2025.(Picha na Ikulu)