Na Mwandishi wetu, Nzega
MKUU wa Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora Naitapwaki Tukai ametoa msaada wa vifaa mbalimbali vya matumizi ya shule kwa wanafunzi ambao ni watoto yatima na wale wenye uhitaji maalum.
DC Tukai akizungumza wakati akigawa vifaa hivyo amesema lengo ni kuhakikisha watoto yatima na wale wenye uhitaji maalum wanapatiwa vifaa vya shule.
Amesema wamegawa baadhi ya vifaa vya shule kwa watoto hao ikiwemo madaftari makubwa na madogo, kalamu, penseli na rula.
Amesema wanampongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kujenga shule na kuanzisha elimu bure kuanzia shule ya awali hadi kidato cha sita hivyo ni wakati wa jamii kusaidia majukumu ya jamii isiyojiweza.
“Tunamshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amejenga miundombinu mbalimbali ya shule sasa ni wakati wa sisi wasaidizi wake kuhakikisha watoto wote wanakwenda shuleni kusoma,” amesema DC Tukai.
Amewapongeza wale wote waliomuunga mkono katika kushiriki kukusanya mahitaji hayo ya shule kwa watoto yatima na wale wenye uhitaji maalum.
“Watoto hao wakasome sasa kwani tumewapatia vifaa hivyo vya shule vutakavyowasaidia kupata elimu kwani watoto wote ni sawa hakuna ubaguzi wanatakiwa wapate elimu,” amesema Tukai.
Amesema baada ya kusimamia ujenzi wa madarasa ya shule mbalimbali na kukamilika sasa ni wakati wa kuhakikisha watoto wote wa kike na wakiume wanakwenda shuleni.