Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Omar Said Shaaban (kulia)akikunjuwa Kitambaa kuashiria Uwekaji wa Jiwe la Msingi Maabara ya Utafiti wa Magonjwa ya Wanyama Dole Wilaya ya Magharibi A .Ikiwa ni Shamra shamra za miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar,yenye kauli mbiu :Miaka 61 ya Mapinduzi:Amani Umoja na Mshikamano kwa Marndeleo yetu.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Zanzibar(ZALIRI)Dk,Talib Saleh Suleiman akitoa historia fupi na Mafanikio ya ZALIRI katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi Maabara ya Utafiti wa Magonjwa ya Wanyama Dole Wilaya ya Magharibi A .Ikiwa ni Shamra shamra za miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar,yenye kauli mbiu :Miaka 61 ya Mapinduzi:Amani Umoja na Mshikamano kwa Marndeleo yetu.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Umwagiliaji Maliasili na Mifugo Ali Khamis Juma akitoa maelezo ya Kitaalamu katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi Maabara ya Utafiti wa Magonjwa ya Wanyama Dole Wilaya ya Magharibi A .Ikiwa ni Shamra shamra za miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar,yenye kauli mbiu :Miaka 61 ya Mapinduzi:Amani Umoja na Mshikamano kwa Marndeleo yetu.
Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Omar Said Shaaban akitoa hotuba katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi Maabara ya Utafiti wa Magonjwa ya Wanyama Dole Wilaya ya Magharibi A .Ikiwa ni Shamra shamra za miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar,yenye kauli mbiu :Miaka 61 ya Mapinduzi:Amani Umoja na Mshikamano kwa Marndeleo yetu. (PICHA NA YUSSUF SIMAI,MAELEZO ZNAZIBAR.10/01/2025.)
…………
Na Ali Issa Maelezo 10/1/2025.
Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Omar Said Shabaan amesema ujenzi wa Maabara ya kisasa ya Utafiti wa Magonjwa ya wanyama utasaidia katika kutambua magonjwa yanayo wakwaza wafugaji katika mifugo yao.
Ameyasema hayo huko Dole Wilaya ya Magharibi A Unguja wakati akiweka jiwe la msingi la maabara ya utafiti wa Magonjwa ya Wanyama kuelekea maadhimisho ya miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Amesema ni muda mrefu wafugaji hupoteza mifugo yao kwa kupata maradhi na kupelekea kufa bila ya kutambua nini tatizo lililowasumbua, hivyo uwepo wa mabaara hiyo ni dhahiri itanusuru mifugo hiyo.
“Pamoja na mafanikio yaliopo sekta ya mifugo, wafugaji wanaendelea kuathirika na uhaba wa malisho ya chakula na uwepo magonjwa ya wanyama, maabara hii ya utafiti utasaidia kutambua magonjwa yanayo wasubuwa wanyama kupelekea kufa” alisema Waziri Shabani.
Aidha alifahamisha kuwa taarifa zote za utafiti wa kimaabara kwa mifugo lazima zithibitishwe na zichambuliwe na wataalamu wa kimaabara, ambapo hivi sasa Zanzibar taarifa zote za kitaalamu za utafii wa kimaabara zinafanywa nje ya nchi jambo ambalo huchelewesha kupata matokeo ya uchunguzi.
Alisema kuwepo maabara hiyo Zanzibar utarahisisha utendaji kazi za utafiti na kupata matokeo chanya ya utafiti ambayo husubiriwa na Wizara.
Akitoa taarifa ya Kitaalam Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji na Mifugo, Ali Khamis Juma amesema jumla ya shilingi Milioni 451,280,124 zimetumika katika ujenzi wa maabara na banda la utafiti wa kondoo ambalo linajengwa katika eneo la taasisi unao jengwa na Kampuni ya KIN limited na kusimamiwa na Wakala wa Majengo Zanzibar (ZBA) kwa fedha za Serikali
Taasisi ya utafiti wa mifugo inaendelea kuandaa wafanyakazi wake ili kuweza kufanyakazi katika maabara itakapokuwa tayari, ambapo kwa sasa wafanyakazi wawili wanaendelea na masomo ya shahada ya uzamivu, wafanyakazi watatu wapo wanaendelea na masomo ya shahada za uzamili, wafanyakazi wanne wanaendelea na masomo ya shahada ya kwanza na mfanyakazi mmoja yupo nchini Ujerumani kwa masomo ya muda mfupi wa matumizi ya vifaa vya maabara na imeajiri wafanyakazi wenye fani ya maabara watatu ili kuhakikisha wanapata wataalamu wa kutosha kuhudumia maabara.
Nae mkuu wa wilaya ya magharibi Sadifa Juma Khamis mapema akitoa salamu za Mkoa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustafa alishukuru Serikali ya awamu ya nane kwa juhudi kubwa inayo chukuwa kuhakikisha sekta ya mifugo inapiga hatua kubwa ya kimaendeleo ili kuona uzalishaji wa mbegu bora za wanya na utabibu wamifigo unapiga hatua.
Ujenzi wa maabara hiyo utafanyika kwa awamu mbili, awamu ya kwaza unahusisha uwekaji wa jiwe la msingi, awamu ya pili utaanza baada ya kukamilika na kuanza kazi kwa maabara hiyo ambapo ni jengo la ghorofa moja litakalokuwa na maabara tatu ndani yake ambazo ni maabara za utafiti wa vidudu vya magonjwa (microbiology research laboratory), maabara ya utafiti wa minyoo na wadudu(parasitology research laboratory) pamoja na maabara ya utafiti wa chakula na lishe (nutrition research laboratory).