Na Mwandishi Wetu
KATIBU Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM)Jokate Mwegelo amesema jumuiya hiyo imeridhishwa na kazi kubwa na nzuri iliyofanywa na vijana wa chama hicho ya kuandaa ukumbi kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa CCM .
Mkutano huo unatarajia kufanyika Januari 18 hafi 19 mwaka huu jijini Dodoma na utaongozwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa,Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza leo Januari tisa jijini Dodoma baada ya kukagua kaz iliyofanywa na vijana wa jumuiya hiyo kuandaa ukumbi , Katibu Mkuu Jokate Mwegelo amesema wao kama vijana wa chama wameridhishwa na maandalizi ya mkutano huo.
“Tumekuja kukagua na kujionea kazi iliyofanywa na vijana wetu wa mkoa wa Dodoma wakiongozwa na Mwenyekiti wa Mkoa na Katibu wa mkoa .
“Chama chetu kina vijana wenye fani tofauti tofauti na wamedhihirisha kwa kazi waliyoifanya katika kufanya maandalizi kuelekea Mkutano Mkuu, hivyo sisi kama viongozi tumeridhishwa na kazi kubwa na nzuri iliyofanywa na vijana wetu.
“Tunaendelea kukishukuru Chama chetu kwa kuendelea kutuamini sisi vijana katika kufanikisha maandalizi ya mkutano mkuu wa Chama Cha Mapinduzi,”amesema Jokate.