Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (Kulia), akiagana na Balozi wa Korea nchini Tanzania, Mhe. Eunju Ahn, baada ya kikao chao jijini Dodoma, ambapo walijadiliana mambo mbalimbali ya ushirikiano wa kiuchumi ikiwemo miradi mbalimbali ya maendeleo, kikao kilichohudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamisi Shaaban na Viongozi wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (Katikati) akizungumza jambo wakati wa kikao chake na Balozi wa Korea nchini Tanzania, Mhe. Eunju Ahn (hayupo pichani) jijini Dodoma, ambapo walijadiliana mambo mbalimbali ya ushirikiano wa kiuchumi ikiwemo ufadhili wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Wengine katika picha ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamisi Shaaban (watatu kulia), Kamishna Msaidizi Idara ya Sera anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Masuala ya Kodi, Bw. Juma Mkabakuli (wa tatu kulia) Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Patrick Pima (wa pili kushoto), na Maafisa wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (Kulia), akimkabidhi zawadi ya baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya hapa nchini, Balozi wa Korea nchini Tanzania, Mhe. Eunju Ahn, baada ya kikao chao jijini Dodoma, ambapo walijadiliana mambo mbalimbali ya ushirikiano wa kiuchumi ikiwemo ufadhili wa miradi mbalimbali ya maendeleo, kikao kilichohudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamisi Shaaban na Viongozi wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (wa sita kushoto) na Balozi wa Korea nchini Tanzania, Mhe. Eunju Ahn (wa tano kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamisi Shaaban (wa sita kulia), Kamishna Msaidizi Idara ya Sera anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Masuala ya Kodi, Bw. Juma Mkabakuli (wa tano kulia), Msaidizi wa Balozi wa Korea, Bw. Sugnyun Lee (wa nne kushoto), Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Patrick Pima (wa nne kulia), na Maafisa wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, baada ya kumalizika kwa kikao chao, jijini Dodoma, ambapo walijadiliana mambo mbalimbali ya ushirikiano wa kiuchumi ikiwemo miradi mbalimbali ya maendeleo. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma)