Na Ali Issa Maelezo 07.01.2025
………….
Waziri wa Maji nishati na madini Shaibu Hassan Kaduara amesema Habari ni nguzo muhimu kwani huuchochea maendeleo ya haraka katika nchi.
Ameyasema hayo Leo huko Tunguu wakati alipokuwa akiweka jiwe la msingi la ofisi ya Shirika la Magazeti ya Serikali Zanzibar kufuatia shamrashamra za kutimiza miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Amesema waandishi kwa kutambua hilo wachuukue nafasi kuandika habari za kimaendeleo ambazo zitachochea maendeleo ya Nchi na kutambua mambo yanayofanywa na Serikali yao.
“Serikali imekua ikuimarisha sekta ya Habari kwa kuweka mazingira wezeshi kwa vyombo binafsi na Serikali kwa kujenga jengo la kisasa ili kuona sekta ya Habari inapiga hatua kubwa ya kimaendeleo, hivyo kuweni wazalendo kusambaza na kuandika Habari njema za kimaendeleo” alisema Mhe. Kaduara.
Aidha amesema kuwa wandishi wandike habari kwa kufuata maadili ya uandishi kwa maslahi ya Nchi pamoja na kuandika habari za Vijijini kwani kuna maendeleo mengi yaliyofanywa huko ambayo yanatakiwa kutambuliwa na wananchi walio wengi.
Amewataka waandishi kutumia kalamu zao vizuri katika uandishi wa taarifa kwani wananchi wanataka kusikia habari kutoka kwao kwa kujuwa yanayotokea nchini.
Nae Katibu Mkuu Wizara ya Habari utamaduni na Michezo Fatma Hamadi Rajab amesema kuwa ujenzi wa ofisi hiyo ni mradi wa miezi 18 unajengwa na Kampuni ya Sky Words Construction limited na kusimamiwa na Wakala wa Majengo Zanzibar (ZBA).
Amesema ujenzi huo uliaza machi 2024 ukiwa na ghorofa 4 nyumba mbili za wafayakazi jengo la Kiwanda cha kuchapisha magazeti ukumbi wa mikutano ambao unachukua watu 150, zitakazoishi familia 8, ofisi za wafanyakazi, jengo la janareta, msikiti, nyumba ya walinzi, ambao unatarajiwa kumaliza Septemba 2025, ukigharibu Bilioni 8.1 saba ambapo mpaka sasa ujenzi huo umetumia miezi minane na kufikia asilimia 50.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayuobu Muhamed Mahmud amesema katika Mkoa wake miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar yamepeleka miradi yenye thamani ya zaidi ya bilioni 100 na miradi 94 imefunguliwa na kuwaekewa jiwe la msingi, pongezi ziende kwa viongozi Majemedari waliopigania uhuru wa Zainzibar.