Mabigwa wa Ligi Kuu NBC Tanzania Bara Yanga Sc imefufua matumaini ya kufuzu hatua ya robo fainali ya ligi ya Mabingwa Barani Afika baada ya kushinda mabao 3- 1 dhidi ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika mchezo wa Kundi A uliochezwa leo Januari 4, 2024 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.
Haikuwa kazi nyepesi kwa mabigwa hao wa Tanzania kwani dakika ya 16 TP Mazembe walifanikiwa kupata bao kwa njia ya mkwaju wa penati lililofungwa na Kipa Msenegal Alioune Badara Faty kufatia beki Mkongo Chadrack Issaka Boka kumchezea rafu beki wa Kimataifa wa Mauritania Ibrahima Keita mzaliwa wa mali.
Hata hivyo mshambuliaji mzawa Clement Francie Mzize alifanikiwa kushinda mabao mawili dakika 33 na 60, huku bao la tatu likifungwa na kiungo wa Kimataifa wa Burkina Faso Stephane Aziz Ki dakika ya 56.
Kwa ushindi huo Yanga SC inafikisha pointi nne na kusongea nafasi ya tatu na kuishusha TP Mazembe nafasi ya nne wakiwa na pointi mbili.
Al Hilal Omdurman inaendelea kuongoza kundi A wakiwa na pointi tisa, ikifatiwa na MC Alger yenye pointi nne na wastani mzuri wa mabao zaidi ya Yanga SC baada ya wote kucheza mechi tatu.
Leo saa 4 :00 usiku MC Alger watawakalibisha Al Hilal Omdurman katika mchezo wan ne wa kundi hilo utakaopigwa dimba la Cheikha Ould Boidiya jijini Nouakchott nchini Mauritania.