Nahodha wa timu ya Mpira wa Miguu Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) Nabby Juma (kulia) akijaribu kumpiga chenga beki wa timu ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke katika mchezo wa kirafiki uliochezwa Disemba 28, 2024 katika Uwanja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) uliopo Mivinjeni, Dar es Salaam, katika mchezo huo walifanikiwa kutoka sare ya bao moja kwa moja (PICHA NA NOEL RUKANUGA)
Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke Mhandisi Ezekiel Mashola (Wa pili kutoka kulia) akiwa na wafanyakazi wa Shirika hilo wakiangalia mechi ya kirafiki kati ya ZECO na TANESCO Mkoa wa Temeke.
Timu ya Mpira wa Miguu Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke wakiwa katika picha ya pamoja.
Timu ya Mpira wa Miguu Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) wakiwa katika picha ya pamoja.
Wachezaji wa mpira wa miguu timu ya TANESCO) Mkoa wa Temeke na Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) wakiwa katika picha ya pamoja.
Wafanyakazi wa TANESCO Mkoa wa Temeke na Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) wakiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa mpira wa miguu.
Picha za matukio mbalimbali.
…..
Timu ya Mpira wa Miguu Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke imetoa sare ya bao moja kwa moja na timu ya Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) katika mchezo wa kirafiki uliochezwa leo Disemba 28, 2024 katika Uwanja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) uliopo Mivinjeni, Dar es Salaam.
Katika mchezo huo wa kirafiki ulikuwa na lengo la kuboresha afya pamoja na kudumisha umoja na ushirikiano jambo ambalo litasaidia kuleta tija katika utendaji.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke Mhandisi Ezekiel Mashola, amesema kuwa kupitia michezo mbalimbali wafanyakazi wataboresha afya zao pamoja na kuendelea kujenga umoja katika kutekeleza shughuli mbalimbali za shirika.
“TANESCO Mkoa wa Temeke tukiwa na timu yetu pamoja na timu ya Shirika la Umeme la Zanzibar tunacheza mechi ya kirafiki kwa lengo la kujenga mahusiano mazuri na kuimarisha Afya” amesema Mhandisi Mashola.
Mhandisi Mashola amesema kuwa ushirikiano huo ni mzuri hivyo mwanzoni mwa mwaka 2025 wanatarajia kwenda Zanzibar kucheza mechi ya kirafiki na ZECO kwa ajili ya kuimarisha mahusiano hayo ambayo yanakwenda kuongeza tija katika utendaji.
Mkuu wa Utawala Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) Bw. Hemedi Khamis Nyoni, amesema kuwa lengo la kushiriki michezo na TANESCO Mkoa wa Temeke ni kujenga undugu pamoja na kubadilishana uzoefu.
Nahodha wa timu ya ZECO Nabby Juma pamoja na timu ya TANESCO Mkoa wa Temeke Magesa Juma, wamefurahisha na utaratibu wa shirika kuweka ratiba ya michezo, huku wakieleza kuwa michezo ina faida nyingi ikiwemo kuhamasisha utendaji wa kazi pamoja na kuimarisha mahusiano kati ya Zanzibara na Bara.