Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea kutoka kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Palamagamba Kabudi tuzo ya kutambua mchango wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuwezesha tasnia ya mchezo wa ngumi nchini, kwenye tukio maalum la pambano la ngumi la ‘Knockout ya Mama’ linalofanyika katika ukumbi wa Super Dome, Masaki jijini Dar es Salaam, Desemba 26, 2024. Kulia ni Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Jerry Silaa na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimvisha Mtanzania Salmin Kassim Mkanda wa ubingwa wa WBF baada ya kushinda pambano dhidi ya mfilipino, Adrian Lerasan kwenye tukio maalum la pambano la ngumi la ‘Knockout ya Mama’ linalofanyika katika ukumbi wa Super Dome, Masaki jijini Dar es Salaam, Desemba 26, 2024.Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidi Bondia Salmin Kassim kitita cha Shilingi Milioni Tano za ‘Knockout ya Mama’ baada ya kuibuka mshindi kwa kutwaa ubingwa wa WBF baada ya kushinda pambano dhidi ya mfilipino, Adrian Lerasan, kwenye tukio maalum la pambano la ngumi la ‘Knockout ya Mama’ linalofanyika katika ukumbi wa Super Dome, Masaki jijini Dar es Salaam, Desemba 26, 2024. Kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Palamagamba Kabudi na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidi Bondia Mtanzania Mchanza Yusuph kitita cha Shilingi Milioni Tano za ‘Knockout ya Mama’ baada ya kuibuka mshindi kwa kutwaa ubingwa wa WBF baada ya kushinda pambano dhidi ya mfilipino, Miel Fajardo, kwenye tukio maalum la pambano la ngumi la ‘Knockout ya Mama’ linalofanyika katika ukumbi wa Super Dome, Masaki jijini Dar es Salaam, Desemba 26, 2024. Kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Palamagamba Kabudi na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akishuhudia mpambano kati ya Mtanzania Mchanza Yusuph na Mphiliponi Miel Fajardo, Katika pambano hilo Yusuph alimshinda. Pambano hilo ni sehemu ya tukio maalum la pambano la ngumi la ‘Knockout ya Mama’ linalofanyika kwenye ukumbi wa Super Dome, Desemba 26, 2024 Masaki jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Jerry Silaa, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Palamagamba Kabudi na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza kwa njia ya Simu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan alipopiga simu kuzungumza na wadau na Mashabiki wa mchezo wa ngumi, wakati wa tukio maalum la pambano la ngumi la ‘Knockout ya Mama’ linalofanyika katika ukumbi wa Super Dome, Masaki jijini Dar es Salaam, Desemba 26, 2024 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza wakati wa tukio maalum la pambano la ngumi la ‘Knockout ya Mama’ linalofanyika katika ukumbi wa Super Dome, Masaki jijini Dar es Salaam, Desemba 26, 2024 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
……………..
*Rais Dkt. Samia apiga simu, awataka mabondia Watanzania kuibeba bendera ya Tanzania kwenye tukio hilo
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo kuhakikisha inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuwawezesha mabondia kunufaika na vipaji vyao.
Ametoa Wito huo jana (Alhamisi, Desemba 26, 2024) wakati wa tukio maalum la pambano la ngumi la ‘Knockout ya Mama’ linalofanyika katika ukumbi wa Super Dome, Masaki jijini Dar es Salaam.
“Awali michezo hii ilikuwa ni ridhaa, lakini kwasasa tumeweka sheria ambazo zinataka mchezo huu uwe wa kulipwa, ambayo mchezaji akiitwa na kuweka mikataba ni lazima apate maslahi”
Aidha, Mheshimiwa Majaliwa ameitaka Wizara hiyo kwa kushirikiana na wadau wa mchezo wa ngumi kuendelea kuhakikisha wanatoa mafunzo bora kwa makocha na wachezaji. “Hii itawezesha kuwa na uhakika kwamba mabondia wa Kitanzania wanapata ujuzi wa kisasa na wanaendelea kufanya vizuri zaidi”.
Katika Hatua Nyingine, Waziri Mkuu ameitaka Wizara hiyo kushirikiana na wadau wa mchezo wa ngumi, wahakikishe wanawake wanapatiwa fursa zaidi ili waweze kushiriki na kuonesha vipaji vyao kwenye michezo hii ya ngumi.
Halikadhalika Mheshimiwa Waziri Mkuu amesema kuwa Sekta ya Michezo imefanyiwa maboresho makubwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambayo imewawezesha Watanzania kushiriki kikamilifu katika michezo mbalimbali
Akizungumza kuhusu tukio hilo la Knockout ya Mama, Mheshimiwa Majaliwa amesema kufanyika kwa tukio hilo kunatokana na kazi kubwa na ushirikiano wa wadau mbalimbali wenye nia ya kusaidia maendeleo ya jamii hasa mchezo wa ngumi.
Naye, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Palamagamba Kabudi amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan mchango mkubwa ambao ameendelea kuutoa katika sekta ya michezo. “Utashi mkubwa wa Kisiasa wa Mheshimiwa Rais umeleta msukumo chanya na kuongeza ari na kuchochea ukuaji wa sekta hii”.
Katika tukio hilo Rais, Dkt. Samia alipiga simu na kuzungumza na Wadau na mashabiki wa mchezo wa ngumi na kuahidi kuwa Serikali itaendelea kuweka mikakati ya kukuza sekta hiyo “Najua wapo mabondia wa nje, sasa Watanzania ibebeni bendera ya Tanzania”