Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kuishi kwa kutunza tunu za upendo, umoja, amani na kufanya matendo ya huruma.
Bashungwa ameeleza hayo wakati alipoungana na waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Kiruruma katika Ibada ya Krismasi, leo tarehe 25 Disemba 2024.
“Tukipendana tutakuwa wamoja, tukipendana tukawa wamoja tutakuwa na amani, lakini kuna tunu nyingine ya ujirani mwema na kufanya matendo ya huruma” amesema Bashungwa
Bashungwa amesema kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na taasisi za kidini likowemo Kanisa Katoliki ambalo ni miongoni mwa Makanisa yenye mchango mkubwa katika kuwakumbusha Watanzania kuishi kwa upendo na amani.
“Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kushirikia na na taasisi za dini likiwemo Kanisa letu Katoliki kwa kuwa ni miongoni mwa makanisa yanafundisha Watanzania kuwa raia wema” amesisitiza Bashungwa
Awali, Paroko Msaidizi wa Parokia ya Kiruruma, Padre Salapioni Mberwa amewaaea Waumini wa Kanisa Katoliki kuiadhimisha Sikukuu ya Krismasi kwa kukumbuka upendo wa Mwenyezi Mungu kwa Wanadamu.
“mahala penye upendo kuna umoja, tunaposherekea Noeli hii, tuenzi umoja na upendo wa Mwenyezi Mungu anaotupatia, mahali penye umoja ndipo penye amani” amesema Padre Salapioni.