Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro KIA na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu ambapo leo ljumaa Disemba 20, 2024, Mhe. Waziri Mkuu anatarajiwa kuzindua tuzo ya kwanza ya uhifadhi na utalii nchini.
Uzinduzi wa tuzo hizo zilizoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii unafanyika Kwenye Hoteli ya Mount Meru.
Tuzo hizo zinalenga kutambua mchango wa watu na Taasisi binafsi zilizochangia mafanikio ya sekta hiyo.