Na. Mwandishi Wetu, Dodoma.
ZAIDI ya Watu 50 wamenusurika kwenye ajali baada ya basi Kampuni ya Urafiki linalofanya safari za Hombolo hadi Stendi ya Job Ndugai kupata ajali Leo majira ya Saa 12:30 asubuhi likitokea Hombolo.
Basi hilo ni lenye namba za usajiri T.886 BYB huku chanzo kikitajwa ni kufyatuka kwa tairi baada ya vyuma kusagika kutokana na ubovu wa miundombinu ya barabara .
Aidha, baadhi ya manusura wamesema kuwa mara nyingi mabasi yanayofanya safari za Hombolo huwa hayakarabatiwi mara kwa mara pia wakiiomba Serikali kuboresha miundombinu ya barabara.
“Mabasi ya huku huwa hayafanyiwi Service na ukiunganisha na miundombinu ya barabara mibovu ina matuta lazima gari liharibike ni muhimu Serikali kuboresha miundombinu ya barabara maana Hombolo ni sehemu ya Jiji na kuna Chuo cha Serikali za Mitaa Wanachuo kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania wanakuja kusomea uongozi hapa lakini pia kuna Taasisi ya Kilimo, kuna bwawa kubwa ambalo linaweza kuwa beach ya Dodoma ,kuna migodi ya madini ya kutengeneza betri lakini miundombinu ya barabara bado sifuri na tuna miaka 63 ya Uhuru”amesema mmoja wa manusura.
Hata hivyo, katika ajali hiyo hakuna hata mmoja aliyejeruhiwa wa kifo ambapo abiria wote wamefaulishwa katika basi jingine la Kampuni hiyo kwenda Stendi ya mabasi Ndugai.