Na Hellen Mtereko, Mwanza
Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza linawashikiria wanaume wawili kwa tuhuma za mauaji ya wake zao huku chanzo cha mauaji hayo kikitajwa kuwa ni wivu wa mapenzi.
Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Polisi Mkoani humo Naibu Kamishna wa Polisi (DCP), Wilbroad Mutafungwa wakati akitoa taarifa za matukio mbalimbali kwa waandishi wa habari.
Amesema Disemba 14, 2024 mtaa wa Nyagungulu katika Wilaya ya Ilemela kulipatikana mwili wa marehemu Leticia Samweli (46) mkulima aliyeuawa na mume wake aitwae Cornelio Kuboja (39) mvuvi ambapo mtuhumiwa amekamatwa na taratibu za kisheria zinaendelea.
Aidha, amesema Wella Mayunga (48) mkulima na mkazi wa Kijiji cha Jojiro aliuawa kwakushambuliwa na mume wake Makoye Machiya (49)