Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dkt. Venance Mwasse (kushoto) akizungumza jambo na Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Dkt. Islam Salum wakati alipofika Ofisi kwake Zanzibar kwa ajili kikao kazi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dkt. Venance Mwasse (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Kamishina wa Magereza Zanzibar Khamis Khamis baada ya kufanya kikao kazi ambacho kimelenga kufanikiza azima Magereza Zanzibar kuachana na matumizi ya kuni na kutumia nishati safi ya kupikia ya Rafiki Briquettes.
……
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dkt. Venance Mwasse amefanya mkutano na Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Dkt. Islam Salum pamoja na mambo mengine wamejadili namna wanavyoweza kuisaidia jamii visiwani Zanzibar kufikiwa na nishati kupikia ya Rafiki Briquettes kwa kuzingatia sasa nchi inatarajia kuanza kupiga marufuku uzalishaji wa kuni na mkaa ili kutekelezaji wa sera ya nishati safi na salama.
Sambamba na mkutano huo katika kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ambaye ni kinara wa matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia Mkurugenzi wa STAMICO amefanya mazungumzo na Kamishina wa Magereza Zanzibar
Khamis Khamis ili kufanikiza azima yao yakuachana na matumizi ya kuni na kutumia nishati safi ya kupikia ya Rafiki Briquettes.
Kwa upande wake Kamishina wa Magereza amemshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO kwa kufika ofisini kwake na kuonesha nia kuisaidia Magereza kuhamia katika matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia ya Rafiki Briquettes, huku akiahidi kutekeleza yote yaliyoelezwa ili Magereza ya Unguja na Pemba kunufaika na nishati ya RafikiBriquettes.
Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt.Venance Mwasse alikuwa Zanzibar kufuatia mualiko Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar.