…..
Happy Lazaro, Arusha .
Serikali kwa kushirikiana na Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa( FAO ) wamezindua Mpango elekezi wa Urejeshaji uoto wa Asili au Misitu Afrika (AFR 100) utakaotekelezwa katika wilaya mbili za Monduli na Karatu kwa Tanzania Bara pamoja na Zanzibar .
Akizindua Mradi huo mkoani Arusha ,Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Arusha Daniel Loirumbe amesema kwamba Mradi huo unalenga kuishirisha Jamii katika kutunza Mazingira na kuongeza thamani ya mazao ya misitu.
Amesema zaidi ya hekta 5.2 milioni kwa Upande wa Tanzania Bara na hekta 25.1 elfu kwa Upande wa Zanzibar zitafanyiwa Kazi ili kurudisha uoto wa Asili ulionza kupotea kutokana na matumizi ya shughuli za kibinadamu.
“Kila mwaka Karibu hekta elfu 400,000 zinapotea hapa nchini kwa shughuli za kibinadamu ikiwemo matumzi ya nishati chafu ya kupikia mkaa na Kuni hivyo tuliazimia kurejesha hekta 5.2 million ya uoto wa Asili kote nchini zilizoharibiwa eidha kwa matumizi ya Ardhi Kilimo na kuharibu Mazingira”amesema .
Naye Afisa Mdhamini Wizara ya Kilimo umwagiliaji maliasili na mifugo Zanzibar Mhandisi Idriss Hassan Abdullah amesema Mradi wa kurudisha maeneo yaliyoharibika ya misitu ambayo yameandaliwa na FAO kwa kushirikiana na nchi ya Ujerumani na haya ni matunda mazuri ya uongozi wa JMT na SMZ chini ya Marais Samia Suluhu Hassan na Dkt.Hussein Ally Mwinyi.
Amesema kwamba viongozi hao wametoa Mazingira mazuri kwa wadau wa mashirika ya maendeleo kufanyakazi zao kwa Mradi huo kuangazia maeneo matatu Karatu Monduli na Zanzibar kwani hata sisi Upande wa visiwani tumeathirika ukatwaji au uharibifu wa misitu ikiwemo ukatwaji wa mkaa, uchimbaji wa mawe, mchanga na ukatwaji wa mikoko na vyanzo vingine vya uharibifu
“Kwa hiyo chini ya Mradi huu tunaweza ufadhili wa fedha kidogo kwa ajili ya kupata urejeshaji wa maeneo yalioharibika ambapo Jamii zenyewe zitakuwa zimeshiriki katika kusimamia maeneo hayo na kuyarudishia wakisaidiwa na serikali na Mradi wenyewe na hilo linafaida Kubwa sana kwa Jamii yetu kama Tanzania na faida ya Moja kwa Moja kwa Jamii husika katika Mradi utakapo fanyika kwani watajipatia kipato kwa faida ya Moja kwa moja”amesema .
Kwa Upande wake Afisa Tawala Mkuu Tamisemi Bernard Urassa kwa niaba ya Katibu Mkuu Tamisemi amesema Mradi huu unawalenga watu wa kada ya chini kuongeza thamani ya uzalishaji na utuzaji wa Mazingira kwa mazao ya misitu nchini kwani hapa nchini uharibifu wa Ardhi ni sawa na asilimia 14 ya Ardhi yote Lengo ni kurejeshwa kwa uoto wa Asili uliopotea.