Happy Lazaro,Arusha .
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa nishati ,Dokta Dotto Biteko amewataka wataalamu wa ununuzi na Ugavi nchini kuwa waadilifu katika utendaji kazi wao sambamba na kukataa rushwa .
Ameyasema hayo leo mkoani Arusha4 wakati akifungua kongamano la 15 la Wataalamu wa ununuzi na Ugavi linalofanyika mkoani Arusha ambalo limeandaliwa na bodi ya wataalamu na ununuzi na Ugavi (PSPTB).
Dokta Biteko amesema kuwa,Taifa linawategemea sana wataalamu hao katika mahala pa kazi hivyo ni lazahakikishe wanakuwa waadilifu na nidhamu.katika.utendaji kazi wao wa kila siku.
Ameongeza kuwa,bodi hiyo imeanzishwa kwa lengo la kupata tija na uwazi katika manunuzi pamoja na kupata bidhaa bora zitakazohusika na kuondoa rushwa katika manunuzi .
“Nawaomba sana hii taaluma yenu ya ununuzi na Ugavi mhakikishe mnaidhamini na mjisimamie wenyewe na swala la uadilifu liwe jambo la kwanza msichukue rushwa ni lazima mheshimu hugo taaluma yenu kwani ni ya muhimu sana .”amesema Dokta Biteko .
Kwa upande wake Naibu Waziri wa fedha Ahmad Chande amesema kuwa,zaidi ya asilimia 70 ya fedha za serikali zinatumika kwenye manunuzi ,hivyo hilo ni eneo kubwa sana na linahitaji umakini wa hali ya juu.
Chande amewataka kuendelea kufanya kazi bila kuogopa chochote na wala wasiogope kulalamikiwa hivyo wafanye kazi na kamwe wasiogope lawama kwani mahali popote unapofanya kazi lazima kuwepo na lawama .
“Nawaombeni sana wataalamu katika ofisi zenu muache wivu,chuki, na husda badala yake mfanye kazi zetu kwa kujituma na mkawe wazalendo katika nchi yenu kwani mnategemewa kwa kiasi kikubwa sana kwenye hiyo nafasi yenu mliyoko nayo. “amesema .
Naye Makamu Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa PSPTB, Benazer Ruta amesema kuwa,bodi hiyo imekuwa na mafanikio makubwa ikiwemo kuendelea kusimamia na kukuza fani ya ununuzi na Ugavi nchini ambapo imeendelea kuhuisha mitaala ya mafunzo ya kitaaluma yenye kujikita katika umahili ili kuzalisha wataalamu wenye ujuzi na umahili katika utendaji katika mnyororo wa ununuzi na ugavi.
Ameongeza kuwa, wameweza kudhibiti ubora wa taaluma hiyo kwa kupitia mitaala ya vyuo na taasisi zingine za elimu ya juu zinazotoa mafunzo ya fani ya ununuzi na Ugavi nchini.