Na Silivia Amandius, Kagera
Mratibu wa TK Movement Mkoa wa Kagera, Ndg. Charlisious Charles, ameongoza uzinduzi rasmi wa mafunzo ya kilimo cha kisasa yaliyofanyika katika Chuo cha Kilimo na Utafiti cha TARI Maruku, Desemba 16, 2024. Mafunzo hayo yamewaleta pamoja vijana kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, huku yakilenga kuwapa maarifa ya kilimo cha kisasa kwa maendeleo yao na jamii.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Ndg. Charles alieleza kuwa mafunzo haya yameanza kwa awamu katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba na yatapanuliwa kufanyika katika wilaya zote za Mkoa wa Kagera. Alifafanua kuwa mpango huu unalenga kuwafikia vijana wote wa TK Movement waliopo katika orodha ya wanufaika wa programu hiyo.
Ndg. Charles alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa juhudi zake za kufungua fursa mbalimbali kwa vijana wa Kitanzania kupitia mafunzo haya. Pia alitoa shukrani kwa Waziri wa Kilimo, Mheshimiwa Hussein Bashe, kwa kuhakikisha vijana wa Kagera wanapata maarifa muhimu yanayolenga kuboresha maisha yao na kuchangia maendeleo ya uchumi wa taifa.
Katibu wa TK Movement Mkoa wa Kagera, Ndg. Mwaija Waziri, aliipongeza TARI Maruku kwa kuandaa mafunzo hayo na kusisitiza kuwa ni msingi wa mabadiliko chanya kwa vijana. Aliwahimiza washiriki kutumia fursa hiyo kupata ujuzi wa kilimo cha kisasa ambacho kinaweza kubadilisha maisha yao na jamii kwa ujumla.
Mafunzo haya ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita kuhakikisha vijana wanajifunza teknolojia za kisasa za kilimo, kuongeza uzalishaji, na kufungua njia mpya za kiuchumi. Viongozi wa TK Movement Mkoa wa Kagera waliwataka vijana wote kushiriki kikamilifu katika mafunzo haya ili kunufaika na fursa zinazolenga kujenga uchumi imara kwao binafsi na kwa jamii kwa ujumla.
Mwisho.
YA KILIMO CHA KISASA TARI MARUKU