Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (Kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa promosheni ya ‘Airtel Santa Mizawadi’ jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa Huduma kwa Wateja, Celina Njuju. Promosheni ya Santa Mizawadi itadumu kwa mwezi mmoja na kutoa fursa kwa wateja na mawakala wa Airtel Tanzania kujizolea zawadi kemkem ikiwemo pocket WiFi, simu janja, pikipiki, runinga na shilingi milioni moja taslim.
Katika kuanza msimu huu wa sikukuu kwa kishindo, Airtel Tanzania imezindua kampeni maalum ya “Airtel Santa Mizawadi,” ikiwa ni njia ya kushukuru na kuwazawadia wateja na mawakala wake wanaoendelea kutumia huduma za Airtel. Promosheni hii kabambe itatoa zawadi mbalimbali ikiwemo pocket WiFi, simu janja, pikipiki, runinga, na pesa taslimu hadi shilingi milioni moja.
Jinsi ya Kushiriki na Kushinda Zawadi za Airtel Santa Mizawadi
Kwa wateja wa Airtel, kushiriki ni rahisi! Unachotakiwa kufanya ni miamala kama kununua bando, kutuma au kupokea pesa, kutoa pesa, kulipa bili, kufanya miamala ya kibenki, kununua muda wa maongezi au vifurushi kupitia 14999#, 15060#, au kutumia My Airtel App.
Kwa mawakala wa Airtel Money, kushiriki kunahusisha kufanya miamala ya kuweka na kutoa fedha kwa wateja. Kila muamala unakupa nafasi ya kuingia kwenye droo za promosheni.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo uliofanyika makao makuu ya Airtel Tanzania, Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Jackson Mmbando, alisema:
“Promosheni ya Airtel Santa Mizawadi inalenga kuonyesha shukrani kwa wateja na mawakala wetu kwa mchango wao mkubwa katika mafanikio ya kampuni. Tunataka kunogesha msimu huu wa sikukuu kwa kuwazawadia zawadi zitakazoboresha maisha yao.”
Mmbando aliongeza kuwa kila muamala unaofanywa na mteja au wakala unazidisha nafasi ya kushinda zawadi hizo nono, akisisitiza dhamira ya Airtel kuendelea kutoa huduma bora zaidi msimu huu wa sikukuu.
Kwa upande wake, Meneja Huduma kwa Wateja wa Airtel, Bi. Celine Njuju, alisema:
“Airtel Santa Mizawadi ni njia yetu ya kuwashukuru wateja na mawakala wetu kwa uaminifu wao. Tunafurahia kuleta tabasamu kwao na familia zao kupitia zawadi hizi. Aidha, balozi wetu maalum, Mr. Santa, atatembelea mitaa mbalimbali nchini kuwazawadia zawadi za papo kwa hapo kwa wateja watakaokutana naye.”
Washindi wa zawadi za Airtel Santa Mizawadi watapatikana kupitia droo za kila wiki na watajulishwa moja kwa moja kupitia namba rasmi ya Airtel, 100.
Kwa taarifa zaidi kuhusu promosheni hii, wateja wanahimizwa kutembelea tovuti ya Airtel au kuwasiliana na huduma kwa wateja kwa kupiga namba 100.
Anza kushiriki sasa na ufurahie msimu huu wa sikukuu ukiwa mshindi wa Airtel Santa Mizawadi!