Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita amekabidhi Fedha taslim Sh.lakini mbili na elfu hamsini kwa lengo kuunga mkono harakati zao wanazozifanya huko Paje Mkoa wa Kusini Unguja.
…………
Mkoa wa Kusini Unguja. 15.12.2024.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita amesema Serikali inajali na kuthamini mchango unaotolewa na Wasanii wa Zanzibar.
Ameyasema hayo mara baada ya kukabidhi fedha taslim kwa Wasanii wa Zenj Fleva na kudansi wakati alipokutana nao katika harakati zao za matangazo ya kampuni ya YAS huko Paje Mkoa wa Kusini Unguja.
Amesema Wasanii hao wana mchango mkubwa kwa Serikali na jamii kwa ujumla hivyo ameahidi kuwaunga mkono Wasanii hao.
Aidha amesema Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ni yao hivyo ni vyema Wasanii hao kuitumia ipasavyo ili kuweza kufikia malengo waliojipangia.
Hata hivyo ameahidi kuwaunga mkono kwa hali na mali sambamba na kuwataka kufanya kazi kwa bidii ili waweze kuelimisha na kuburudisha jamii.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Othman Ali Maulid amesema amefarijika sana kutokana na ziara iliofanywa na Waziri huyo.
Aidha ameahidi kushirikiana kwa hali na mali katika kuwaendeleza Wasanii wa Wilaya ya Kusini.
No Wasanii hao wamemshukuru Waziri huyo na Mkuu wa Wilaya ya kusini kwa kukadhili fedha taslim jambo ambalo limewapa moyo, faraja na kuongeza juhudi ya kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
Waziri Tabia, amekabidhi Sh. laki mbili (200,000) kwa Wasanii wa Zenj Fleva na Kudansi ambapo kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Kusini Othman Ali Maulid amekabidhi Sh. Laki moja na elfu hamsini (150,000) ili kuunga mkono kazi kubwa inayofanywa na Wasanii hao.