BODI ya Ununuzi na Ugavi (PSPTB), imewafutia matokeo watahiniwa wawili ambao walikutwa wakifanya vitendo vya udanganyifu katika kumbi za mtihani ya 29 ya bodi hiyo.
Akizungumza na wandishi wa habari leo, jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa PSPTB, Godfrey Mbanyi, alisema watahiniwa 610 wamefaulu mititihani kati ya watahiniwa 1314 wa Bodi hiyo.
Alisema watahiniwa hao wawili walikamatwa na wasimamizi wa mitihani katika kituo cha Moshi mkoani Kilimanjaro.
“Na baada ya taratibu zote kufuatwa za kiutaratibu wa bodi na baada ya vielelezo kuwakilishwa kwenye bodi ya wakurugenzi kwa kauli moja ya bodi imeridhia kwamba makossa yaliyofanyika kukutwa na mitihani ni makossa ambayo hayakubaliki, kitaaluama, kimaadili na kwa taratibu zote za mitihani kwa hiyo wamefutiwa matokeo.
Adhabu hiyo ya kufutiwa matokeo inaambatana na kusimamishwa kwa kufanya mitihani ya Bodi kwa vipindi vitatu mfululizo kwa mara nyingine watahiniwa hao wawili hawataruhusiwa kufanya mitihani mwezi Mei 25 hawataruhusiwa kufanya mitihani mwezi Novemba 25 wala hawataruhusiwa kufanya mitihani mwezi Novemba 2025.
Alisema nafasi waliyonayo itakuwa ni mwezi Mei 2026 kama bado watakuwa na nia ya kufanya mitihani hiyo.
“Nitowe wito kwa watahiniwa wetu wote kutojihusisha na vitendo vya aina vyovyote vya kudanganya wakati wa mitihani kumbi zetu zote za mitihani zina kamera, hatufanyii mitihani kusiko na kamera za CCTV kwa hiyo kwa yote atakabainika atachukuliwa hatua stahiki ikiwemo hii ya kufutiwa matokeo, kusimamishwa kufanya mitihani.
“Lakini akirudia anaweza akafutiwa kabisa na usajili na asiweze kufanya kazi zozote za ununuzi na ugavi kwa mujibu wa sharia Namba 23 ya mwaka 2007 iliyoanzisha Bodi hii,”alisema Mbanyi.
Aidha, Mbanyi alisema Bodi hiyo ya Wakurugenzi iliidhinisha matokeo ya mitihani ya 29 ya Bodi, mitihani iliyofanyika kuanzia tarehe 11 Novemba mwaka huu 2024.
“Katika mitihani hiyo kulikuwa na watahiniwa 1403 lakini kati ya hao 1314 ndio waliowezakuja kufanya mitihani hiyo wengine kutokana na changamoto mbalimbali za kikazi, kiafya na sababu zingine hawakuweza kujitokeza kuja kufanya mtihani.
“Baada ya mchakato kupita na kufanyika vizuri ufaulu unaonesha kwamba kati ya 1314 walifanya mitihani hiyo waliofaulu ni 610 ambao ni sawa na asilimia 46.4. ambao watakuwa na mtihani ya marudio ni 663 sawa na asilimia 50.1. hawa ni watu ambao wamefaulu baadhi ya masomo, mengine wamefeli.
“Lakini pia wapo watahiniwa 41 hawa wamefeli kabisa masomo yote kwa hiyo watapaswa kurudia masomo ambayo wameka katika ngazi husika ya mtihani.
“Nichukuwe nafasi hii kuwapongeza watahiniwa wote ambao wameweza kufaulu mitihani lakini pia niwashukuru na kuwapongeza waalimu na wakufunzi mbalimbali waliowasaidia watahiniwa wetu katika maandalizi ya mitihani ya bodi ya wataalamu ya manunuzi na ugavi kwa mwaka 2024,”alisema Mbanyi.