Dkt. Tumaini Msowoya akiwa na watoto kutoka Shule ya Msingi Igangidung’u, Wilayani Iringa.
………………
Mwandishi wetu, Iringa
Mkurugenzi wa Msowoya Foundation, Dkt Tumaini Msowoya amesema kila mmoja analo jukumu la kuwalinda watoto dhidi ya vitendo vya ukatili ikiwamo vipigo, ubakaji na ulawiti huku akiwaomba wananchi wa Igangidung’u kuwa mfano.
Dkt Msowoya amesema hayo katika Kijiji cha Igangidung’u, Kata ya Kihanga Wilayani Iringa wakati akichangia mdahalo wa Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia iliyoandaliwa na World Vision kupitia Program ya Kihanga.
“Mtoto wa mwenzako ni wako pia, ukiwalinda ulio wazaa walinde na watoto wenzao. Sisi sote tunalo jukumu la kuwalinda watoto wetu dhidi ya ukatili,” amesema Dkt Msowoya na kuongeza;
“Matukio ya kikatili ni mengi na tunayasikia kila siku. SI wanawake Wala wanaume sote tumejisahau. Malezi ya mtoto ni yetu sote, baba na mama,”
Mdahalo huo ulihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo madiwani wa kata za maboga na Kihanga.