Diwani wa kata ya Luchelele Vicent Tege akipanda mti katika shule mpya ya shadi iliyopo kata ya Luchelele .
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi.
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Luchelele wakiwa wamejitokeza katika zoezi la upandaji miti shule mpya ya shadi.
………..
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza imeadhimisha sherehe za maadhimisho ya miaka 63 ya uhuru wa Tanzania Bara Kwa kupanda miti zaidi ya 5000.
Hayo yamejili baada ya Rais wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania Dkt, Samia Suluhu Hassani kutoa agizo fedha zote zilizotengwa Kwa ajili ya maadhimisho ya uhuru zitumike katika kufanya shughuli za kijamii, ikiwemo upandaji miti, kufanya usafi wa mazingira katika maeneo ya kijamii, utoaji wa misaada katika Kambi za wazee pamoja na wahitaji maalum.
Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi ameeleeza kuwa katika kuadhimisha siku hiyo wamepanda miti katika shule mpya ya msingi Shadi inayojengwa iliyopo kata ya Luchelele, shule ya msingi Buhongwa, Bulale Sekondari pamoja na Hospital ya wilaya ya Nyamagana (BUTIMBA). hb bnz
Amina ameeleeza kuwa upandaji wa miti utasaidia kupata mvua za kutosha, kupunguza mfuliko yanayotokea, pia kusaidia kuondokana na ukame unaoweza kusababisha mvua kutokunyesha pamoja na kupunguza hewa.
“Tunapokosa upandaji miti katika Wilaya yetu ya Nyamagana kunakuwa na ukame na mvua hazinyeshi au wakati mwingine zinakuwa chache lakini pia mvua zinapokuwa chache hatupati chakula Kwa sababu Wilaya yetu pia tunategemea kupata chakula sehemu nyingine” Alisema Makilagi.
Askari Mhifadhi Mwandamizi kutoka Wakala Huduma za Mistu Wilaya ya Nyamagana (TFS), Mahija Mkomwa ameeleza kuwa katika kuazimisha sherehe za miaka 63 ya uhuru wamepanda miti zaidi ya 500 katika shule mpya ya shadi iliyopo kata ya Luchelele.
Kwa upande wake Afisa Mazingira Jiji la Mwanza David Joseph ameeleza kuwa Taifa limeweka mpango wa kupanda miti Kila Wilaya Mil1.5 lakini kutokana na hali ya kimazingira na ongezeko la watu na makazi hivyo kama Halmashauri wanategemea kupanda miti 6000 Kila Mwaka
“Katika swala Zima la kuhifadhi na kutunza mazingira sio la Mkurugenzi, sio la TFS, Wala sio la viongozi ni swala shirikishi Kwa jamii na jamii ni lazima itambue namba Bora ya kuhifadhi na kutunza mazingira Kwa ajili ya naendeleo yajayo” Alisema Joseph.
Mkuu wa shule ya msingi Luchelele ambaye pia ni Msimamizi wa shule mpya Shadi Amani Anyosistye inayojengwa pamoja na wananchi wa kata hiyo wameishukru serikali kupanda miti katika shule ya shadi ambayo itakuwa faida kwa watoto watakaopata nafasi ya kusomea hapo.