Muhifadhi Kiongozi katika Kituo cha Makumbusho na Nyumba ya utamaduni Agnes Robert akizungumza na wahababari baada ya uzinduzi wa program mpya ya vifurushi vya misafara ya kutembelea Makumbusho na Malikale zilizopo nchini msimu huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka katika halfa ambayo imefanyika jijini leo Dar es salaam.
Baadhi ya wanafunzi na wadau mbalimbali walioshiriki katika uzinduzi wa program mpya ya vifurushi vya misafara ya kutembelea Makumbusho na Malikale zilizopo nchini msimu huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka katika halfa ambayo imefanyika jijini leo Dar es salaam.
Picha ya pamoja Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga, pamoja wanafunzi wa Sekondari pamoja na kutoka Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere uzinduzi wa program mpya ya vifurushi vya misafara ya kutembelea Makumbusho na Malikale zilizopo nchini msimu huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka katika halfa ambayo imefanyika jijini leo Dar es salaam.
………………………..
NA MUSSA KHALID
Katika kuadhimisha Miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara,Makumbusho ya Taifa la Tanzania imendelea kutoa elimu kwa jamii ili kurithisha vizazi vya sasa na baadae viendelee kuifahamu histotia ya nchi yao.
Hayo yameelezwa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga wakati akitambulisha uzinduzi wa program mpya ya vifurushi vya misafara ya kutembelea Makumbusho na Malikale zilizopo nchini mbele ya wanafunzi wa Sekondari na Chuo Kikuu ambao wametembelea Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Posta ili kujifunza zaidi katika msimu huu wa mishoni mwa mwaka.
Dkt Lwoga amesema kuwa malengo yao ni kuhakikisha wanawavutia watanzania kutembelea maeneo ya kihistoria ili kujionea program mbalimbali zinazofanyika katika maeneo hayo.
‘Tumeweza kujikumbusha mambo mbalimbali ambayo yalitokea na hasa kuenzi waasisi wa taifa letu wakiongozwa na Hayati baba wa Taifa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere na kuona kwamba pamoja na changamoto ambazo walikumbana nazo hawakukata tama badala yake walihakikisha kwamba taifa letu linapata uhuru mwaka 1961’amesema Dkt Lwoga
Amesema katika kurithisha huko wanakuwa na program mbalimbali za kielimu ikikiwemo burudani na midahalo na mawasilisho kutoka kwa wadau mbalimbali wa historia ya Mkaumbusho na Malikale.
Aidha Dkt Lwoga amesisitiza kuwa kupitia programa ambayo wameizindua leo watanzania wanapaswa kuienzi historia yao ikiwemo ya uhuru kwa kutembelea Makumbusho na Malikale ili kurithisha vizazi vya sasa na vijavyo.
Kwa upande wake Muhifadhi Kiongozi katika Kituo cha Makumbusho na Nyumba ya utamaduni Agnes Robert amesema kuwa ili kuifahamu historia ya nchi kabla ya uhuru na baada ya uhuru ni vyema jamii ikatenga muda kutembelea Makumbusho.
Amewahimiza watanzania kujenga tabia ya kutembelea maeneo haya adhimu ya kihistoria na Malikale kwa kuwa kumeandaliwa programu maalum za kuwapa mafunzo na burudani wazazi na watoto wao kwa bei maalum.
Awali akizungumza Mtoa mada katika hafla hiyo Mfanyakazi kutoka Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Geofrey Malila amesema miaka 63 ya uhuru Taifa limepiga hatua katika masuala ya kiuchumi,kijamii na kiutamaduni huku Mwanafunzi kutoka chuo hicho Clara Joseph akisema kutembelea kwao Makumbusho wameweza kujifunza masuala mengi ya kihistoria.
Hata hivyo Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho amesema Makumbusho ya Malikale ni zaidi ya burudani kwani kuna elimu ya msingi inayojenga uzalendo,historia yake na mtoto kujitambua kuweza kupata uiamara wa kuweza kuelewa historia yake na dunia katika masuala mbalimbali ya uongozi na shule.