Bondia wa Ngumi za Kulipwa Twaha Kiduku akiwa katika mbio za KM 30 zilizoandaliwa na Bondwa Hiking Club,Jeshi la Polisi na Mahakama Kuu kanda ya Morogoro
Mbio zikendelea.
…….
Klabu ya wapanda milima ya Bondwa Hiking ya Mkoani Morogoro kwa kushirikiana na mahakama kuu kanda ya Morogoro pamoja na jeshi la Polisi Mkoani humo limefanya mazoezi ya pamoja katika kuelekea maadhimisho ya miaka 63 ya uhuru wa Tanganyika (Tanzania)
Lengo jingine la mazoezi hayo ya pamoja ambayo ilikuwa ni kukimbia kilometa 30 kwa mbio ndefu huku wale wa mbio fupi wakitembea nakukimbia KM 15 kuhamashisha ufanyaji wa mazoezi,ulaji mzuri wa chakula wenye kuzingatia kanuni za lishe bora kwa afya ya akili na mwili
Mgeni rasmi katika tukio hilo alikuwa ni kamanda wa polisi Morogoro SACP Alex Mkama, amewapongeza walioshiriki ikiwa pamoja na bondwa Hiking kwa kuweza kushirikiana nao katika kuratibu tukio hilo
Kamanda Mkama amesema kuwa matukio kama hayo yanaongeza hamasa kwa wananchi kuwa karibu na jeshi hilo hali ambayo itasaidia kupambana na vitendo vya kihalifu katika jamii.
Akizungumza na wanahabari Mwenyekiti wa Klabu hiyo ya Bondwa Wakili Msomi Godfrey Mwansoho amesema kuwa wameamua kuandaa tukio hilo kuadhimisha miaka 63 ya uhuru huku pia kuadhimisha mwaka mmoja wa klabu hiyo ambayo ilianzishwa desemba 9,2023
Aidha amesema kuwa katika tukio hilo wamekwenda sambamba na uzinduzi wa klabu ya mazoezi chuo kikuu cha Jordan (JUCo Jogging Club)
Akizungumza kwa niaba ya mahakama kuu kanda ya Morogoro Mtendaji wa mahakama hiyo Ahmed Suleiman Ng’eni amesema uwepo wa mazoezi ya pamoja unasiadia ukaribu baina ya viongozi na watumishi wao huku pia kwa jeshi la polisi kupata taarifa za uhalifu mapema
Mbio hizo zimeshirikisha wadau mbalimbali akiwepo Bondia maarufu nchini Twaha Kidudu,klabu ya mazoezi ya Turiani Jogging ya wilayani Mvomero, kituo cha mafunzo ya Taekwondo Morogoro, wanafunzi wa chuo cha Jordan na wananchi wa mkoa wa Morogoro.