NA VICTOR MASANGU,KIBAHA
Halmashauri ya Kibaha mji iliyopo Mkoa wa Pwani kesho inatarajia kuzindua rasmi soka jipya la kisasa linalojulikana kama (Kibaha Shoping Moll) Novemba 7 mwaka huu lililogharimu kiasi cha shilingi bilioni 7.
Akizungumza na waandishi wa habari Afisa mapato wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha Luna Kakuru amebainisha kwamba mradi huo ni kati ya miradi ya kimkakati na kwamba fedha hizo zimetolewa na Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan
Luna amesema kwamba katika mradi huuo wanategemea baadae mapato kuongezeka zaidi kutokana na huduma zitakazoendelea kutolewa ikiwepo maeneo ya maegesho ya magari.
Naye Afisa Masoko wa soko hilo Sabrina Kikoti amesema katika ufunguzi huo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson John na kwamba soko hilo litakwenda kufungua fursa za uchumi kwa wananchi wa Kibaha pamoja na maeneo mengine.
Sabrina ameishukuru Serikali kwa kutoa fedha hizo ambazo zimetekeleza mradi huo unaokwenda kutoa huduma nyingi huduma nyingi ambazo wananchi walikuwa hawazipati kwa wakati.
Amesema katika ufunguzi huo wafanyabiashara mbalimbali wakubwa watashiriki wakiwemo wasanij kutoka ndani na nje ya Mji wa Kibaha.
Nao baadhi ya wafanyabiashara akiwemo Charles Chandika amesema kwamba uwepo wa soko hilo ni fursa kwa wafanyabiashara kutoa huduma mbalimbali kwa wakazi wa mji huo kwa gharama nafuu.
Naye Lidya Vicent mfanyabiasha wa nguo katika soko hilo amesema uwepo wa soko hilo umewawezesha kupata fursa ya mahali sahihi pa kuuzia bidhaa zao.