Na. Mwandishi Jeshi la Polisi Kinondoni Dar es salaam.
Jeshi la Polisi Mkoa wa kipolisi Kinondoni umefanya uzinduzi wa Kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ambao umebeba kauli mbiu isemayo Kuelekea Miaka thelathini ya Beijing
Akizindua kampeni hiyo leo Disemba 06, 2024 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bwana Saad Mtambule ameiomba jamii kuendelea kutoa malezi bora kwa jamii huku akiwasihi kushirikiana na Jeshi la Polisi katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia huku akiitaka jamii kukemea vitendo hivyo.
Ameongeza kuwa ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni itaendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika mapambano ya dhidi ya ukatili wa kijinsia huku akitumia fursa hiyo kulipongeza Jeshi hilo katika mapambano ya ulatili.
Kwa upande wake kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi Kinondoni kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Mtatiro Kitinkwi amesema tayari kesi 25 za vitendo vya ukatili zimefikishwa mahakamani huku akisema kuwa Jeshi la Polisi Mkoa wa kipolisi Kinondoni litaendelea kuwafikisha mahakamani na kutoa elimu kwa makundi mbalimbali katika ili kujenga uwelewa wa pamoja juu ya vitendo vya ukatili vinavyofanywa na baadhi ya watu katika jamii.
Nao baadhi ya wananchi walioshiriki katika kampeni hiyo hiyo licha ya kulishukuru Jeshi la Polisi wamesema kuwa mafunzo na kampeni hiyo iendelee iliitumike kuwakumbusha wananchi juu ya madhara ya vitendo vya ukatili.