Dkt. Yohana Msumba Ambaye hajavaa kofia akipokea Baiskeli kwa ajili ya Kubebea Wagonjwa kutoka kwa Mwakilishi wa kampuni ya Boart Longyear Bonophace Mushongi.
Akiongea Baada ya kukabidhi Vifaa hivyo Mwakikisho wa kampuni ya Boart Longyear Bw. Bonophace Mushongi, alisema wametumia maadhimisho haya mwaka huu kutoa msaada wa vifaa tiba na kushiriki kutoa elimu dhidi ya maambukizi ya Ukimwi.
“Miongoni mwa Vifaa tulivyotoa ni pamoja na seti ya televisheni ambayo itatumika Kuonyesha vipindi vya elimu ya afya lakini hapa ni sehemu inayopaswa kuwa katika mazingira ya usafi wakati wote tumeleta pia vifaa vya kufanyia usafi” ,alisema.
Kwa Upande wake Mganga Mfawidhi wa Kituo hicho Dkt. Yohana Msumba Ameishukuru Kampuni ya Boart Longyear kwa kutoa Vifaa hivyo na kutambua Mchango wa kituo hicho katika Kuwahudumia wananchi