Wazairi wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda akizungumza jambo leo Disemba 4, 2024 jijini Dar es Salaam wakati akihitimisha Kongamano la Tisa la Sayansi, Teknolojia, Ubunifu na Maonesho (STICE 2024), lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Amos Nungu akizungumza jambo leo Disemba 4, 2024 jijini Dar es Salaam wakati wa kuhitimisha Kongamano la Tisa la Sayansi, Teknolojia, Ubunifu na Maonesho (STICE 2024), lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo Husna Sekiboko akizungumza jambo leo Disemba 4, 2024 jijini Dar es Salaam wakati wa kuhitimisha Kongamano la Tisa la Sayansi, Teknolojia, Ubunifu na Maonesho (STICE 2024), lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam.
Baadhi ya Wabunifu wa Sayansi na Teknolojia pamoja na wadhamini wa Kongamano la Tisa la Sayansi, Teknolojia, Ubunifu na Maonesho (STICE 2024) wakipewa vyeti na Wazairi wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda kama sehemu ya kutambua mchango wao katika sekta ya sayansi.
Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Tisa la Sayansi, Teknolojia, Ubunifu na Maonesho (STICE 2024) wakifatilia jambo katika kongamano hilo.
……..
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Wazairi wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema kuwa Serikali itaendelea kuwekeza katika sekta ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu ili kuwawezesha vijana wa kitanzania kuona sekta hiyo kama fursa ya maendeleo.
Akizungumza leo Disemba 4, 2024 jijini Dar es Salaam wakati akihitimisha la Tisa la Sayansi, Teknolojia, Ubunifu na Maonesho (STICE 2024), lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Profesa Mkenda, amesema kuwa mfuko wa samia ambao umezinduliwa katika kongamano hilo umelenga kusaidia wabunifu kwa kuwapatia mitaji ili kuendeleza bunifu zao ziweze kusaidia kuboresha maisha ya jamii na kukuza uchumi wa Nchi.
Profesa Mkenda amesema kuwa ni umuhimu wabunifu kutumia maarifa waliyopata katika kongamano hilo ili kuhakikisha sayansi na ubunifu havibaki kwenye maabara bali kubadilisha maisha ya watazania.
“Serikali itaendelea kutoa msukumo ili kuhakikisha sayansi inakuwa mhimili wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini” amesema Profesa Mkenda.
Amesema kuwa wakati umefika kwa wabunifu kuhakikisha kazi zao zinafika sokoni kwa ajili ya kutatua changamoto za kijamii, huku asisitiza kuwa sio vizuri kazi za wabunifu kila mwaka zinakuwa hizo hizo, hivyo Mfuko wa Samia utaleta tija katika kufikia malengo.
Profesa Mkenda amesema kuwa kongamano hilo limefanyika kwa siku tatu ambalo limebeba kauli mbiu isemayo : Matumizi ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kwa Ustahimilivu wa tabianchi na Uchumi Shidani” limekuwa jukwaa muhimu kwa wataalamu wa sayansi, watafiti na wabunifu katika kubadilishana mawazo na kutafuta suluhisho za changamoto.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo Mhe. Husna Sekiboko, amesema kuwa mapendekezo yaliyotolewa katika Kongamano hilo yanakwenda kufanyiwa na kazi kwa vitendo bungeni ili kuhakikisha yanakuwa na tija kwa manufaa ya Taifa.
“Wasomi wengi wamekuwa wakifanya tafiti kwa ajili ya kutatu tatizo, lakini watekelezaji wamekuwa wakiweka kabatini, katika hili sisi wabunge tunakwenda kusimamia na kushauri ili kuhakikisha yote yaliochakatwa kwa lengo la kutatu changamoto mbalimbali katika Nchi, tutahakikisha serikali inakwenda kutekeleza yaweze kuleta tija inayokusudiwa” amesema Mhe. Sekiboko.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknlojia (COSTECH) Dkt. Amoss Nungu, amesema baadhi ya mapendekezo waliyoyatoa katika Kongamano hilo ni pamoja na kuifanya Teknolojia ya Ubunifu Kukuza Uchumi, kujenga uhusiano na wenye viwanda na kufanya mikutano ya pamoja ya eknolojia ya kukubaliana na mabadiliko ya Tabia nchi.
Amesema kuwa Kongamano hilo lilikuwa na malengo manne ambayo yamefikiwa kwa kiwango kikubwa ikiwemo kuwezesha usambazaji wa utumiaji wa matokeo ya utafiti na bidhaa za ubunifu.
Kuhimiza ushirikiano kati ya watafiti, watenga sera na wadau wa sekta ya viwanda, kuhamasisha nafasi ya sayansi na ubunifu katika kushughulikia changamoto za Kitaifa na Kimataifa katika nyanja za ustamilivu, mabadiliko ya Tabia ya Nchi.
Kuhamasisha kizazi kijacho cha wabunifu wanasayansi kwa kukuza ushiriki wao katika elimu ya sayansi pamoja na ubunifu wa hisabati.
Kongamano hilo limefanyika kwa siku tatu likiongozwa na kauli mbiu “Matumizi ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu katika kuhimuli changamoo za Mabadiliko ya Tabianchi na kuchangia kwenye uchumi shindani”