Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Omar Said Shaabani akisisitiza jambo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Manesho ya Biashara ya Kimataifa ya Kumi na Moja (11)yatakayofanyika kuanzia Tarehe 1 January hadi Tarehe 15 kwa Unguja katika eneo la Nyamanzi na kwa Pemba yataanzia Tarehe 7 hadi 15 katika Eneo la Chamanangwe hafla iliofanyika katika Ofisi ya Wizara hio Kinazini Zanzibar.
Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Omar Said Shaabani (Kushoto)akimsikiliza Mwandishi wa Habari wa ITV Farouk Karim akiuliza maswali katika mkutano wa Waziri na Waandishi wa Habari akizungumza kuhusiana na Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Kumi na Moja (11)yatakayofanyika kuanzia Tarehe 1 January hadi Tarehe 15 kwa Unguja katika eneo la Nyamanzi na kwa Pemba yataanzia Tarehe 7 hadi 15 katika Eneo la Chamanangwe hafla iliofanyika katika Ofisi ya Wizara hio Kinazini Zanzibar.
Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika mkutano wa Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Omar Said Shaabani akizungumza kuhusiana na Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Kumi na Moja (11)yatakayofanyika kuanzia Tarehe 1 January hadi Tarehe 15 kwa Unguja katika eneo la Nyamanzi na kwa Pemba yataanzia Tarehe 7 hadi 15 katika Eneo la Chamanangwe hafla iliofanyika katika Ofisi ya Wizara hio Kinazini Zanzibar.
Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika mkutano wa Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Omar Said Shaabani akizungumza kuhusiana na Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Kumi na Moja (11)yatakayofanyika kuanzia Tarehe 1 January hadi Tarehe 15 kwa Unguja katika eneo la Nyamanzi na kwa Pemba yataanzia Tarehe 7 hadi 15 katika Eneo la Chamanangwe hafla iliofanyika katika Ofisi ya Wizara hio Kinazini Zanzibar.
Mwandishi wa Habari wa ITV Farouk Karim akiuliza maswali katika mkutano wa Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Omar Said Shaabani wakati akizungumza kuhusiana na Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Kumi na Moja (11)yatakayofanyika kuanzia Tarehe 1 January hadi Tarehe 15 kwa Unguja katika eneo la Nyamanzi na kwa Pemba yataanzia Tarehe 7 hadi 15 katika Eneo la Chamanangwe hafla iliofanyika katika Ofisi ya Wizara hio Kinazini Zanzibar. (PICHA NA YUSSUF SIMAI,MAELEZO ZANZIBAR.04/12/2024)
………
Na Ali Issa Maelezo
Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar itaendelea kufanya Maonyesho ya Biashara katika eneo lake la kudumu liliopo nyamazi kwa ajili ya maendeleo ya Nchii na wafanya Biashara wandani na nje ya Nchi.
Waziri wa Wizara hiyo Mhe Omar Said Shabani huko Ofisini kwake kwake kinazini mjini Unguja wakati alipokuwa na mazunguzo na wandishi wa Habari.
Amesema kufuatia Sherehe za maadhimisho ya Mapinduzi ya Zanzibar mwaka huu Zanzibar kila Wizara huratibiwa kuwa na shughuli zake mbali mbali za miradi ya kimaendeleo
Amesema kuwa kwa upande wao mwaka 2025 licha ya kuwepo shughuli hizo za kimaendeleo pia wanatarajia kuwa na maeonyesho ya kibiashara ya Kimataifa yatayo washirikisha wafanya Biashara mbalimbali na wajasiriamali wandani na nje ya Nchi.
Alisema maeonyesho hayo yataaza Junari mosi hadi Januari 15 kwa Unguja na yatashirikisha wafanyabishara na wajasiriamali 500 kwa Unguja na kwa Upande Pemba yanatarajiwa kuaza Januari saba(7) hadi15 katika viwanja vya Chamanangwe na yatashirikisha wafanya Biashara na wajasiriamali 100 na kuwataka wafanya bishara kwenda kujisajili.
Alifahamisha kuwa maeonyesho hayo ni upatikanaji frusa za masoko kwa wafanya Biashara kwani watapata nafasi ya kuuza bidhaa zao na kuzitangaza kitaifa na kimataifa.
Pamoja na hayo alisema kuwa wanadhamira ya kuwapatia semina wafanya Biashara ili kufanya biashara zao zaidi kimtandao na kidijitali njia ya kisasa ya kuuza bidhaa kidijitali na kuzitangaza katika masoko duniani.
Aidha alisema mwaka huu wametoa ofa maalum ya punguzo la asilimia kumi (10) kwa Jumuiya ya wafanyabishara wanawake ambao wamejisajili na wamesajiliwa na Jumuiya hiyo ikiwa ni kuwapa hamasa zaidi kufanya biashara.
Maeonyesho hayo ya 11 ambapo kauli mbiu yake kwa mwaka huu Biashara mtandao kwa maendeleo ya Biashara na uwekezaji.