Ikiwa ni mwendelezo wa utoaji elimu kwa makundi mabalimbali katika jamii kikosi cha wanamaji dawati la jinsia na watoto limewafikia watumiaji wa vyombo vya majini na kuwapa elimu ya ukatili ikiwa ni pamoja elimu ya usafirishaji haramu wa binadamu.
Akiongea wakati wa utoaji elimu hiyo iliyofanyika katika bahari ya hindi Mkuu wa dawati la Jinsia na watoto kutoka kikosi cha wanamaji Jeshi la Polisi Mkaguzi wa Polisi Avelina Temba amesema kuwa umekuwa ni utaratibu wa dawati hilo kuyafikia makundi hayo nakuyapa elimu ili kujenga uelewa wa pamoja juu ya vitendo vya unyanyasaji na ukatili.
Mkaguzi wa Polisi Shafii Lubarati akagusia vitendo vya baadhi ya watu kufanya Biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu ambapo amebainisha kuwa kwa ambae atafanya vitendo hivyo ni kinyume cha sheria na Jeshi la Polisi litamkamata