TAASISI ya Watu wenye Ulemavu(YoWDO),Chama cha Watu wenye Ualbino nchini(TAS),wakishirikiana na Shirika la haki za Kisheria, maendeleo ya jamii na uchumi(DOLASED), wameomba serikali kutoa elimu juu ya mkopo wa asilimia mbili kwa walemavu ilikuondoa ombaomba mitaani.
Awali taasisi hiyo ilisema watu wenye Ulemavu wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo ni vikwazo kwa ushiriki wao katika fursa za uongozi.
Hayo yamesemwa leo Disemba 3,2024 na Mkurungenzi wa Taasisi ya watu wenye Ulemavu, Rajab Mpilipili wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu ofisini kwao Dar es salaam .
“Walemavu wengi wanakuwa ombaomba kutokana na kukosa elimu pamoja na mitaji ya kufanya shughuli za kijamii, Kisiasa na kiuchumi zitakazo ongezea pato la mtu mmoja mmoja na taifa ,lakini pia changamoto kubwa ni mazingira yasiyofikivu, ubaguzi na unyanyapaa na ukosefu wa elimu kwa watu mwenye ulemamu kuhusu mikopo ya asilimia 2,”amesema MpiliPili
Mpilipili amesema jamii ina mtazamo hasi dhidi ya watu wenye Ulemavu hasa kwenye uongozi hivyo kufanya watu hao kushindwa kujiamini kwa kuthubutu kushiriki katika michakato mbalimbali ya uongozi hivyo ni wakati wa vyama vya siasa, taasisi za serikali na jamii kwa ujumla kuondoa vikwazo hivyo ilikuhakikisha mazingira ya Kisiasa yanawakilisha sauti za kila mtu.
Mwakilishi kutoka Chama cha Watu wenye Ualbino(TAS) Abdallah Cheka amesema maadhimisho hayo yaiguse serikali na jamii kuendelea kuimarisha haki za watu wenye Ualbino kwa kukomesha mauaji,manyanyaso na ukatili.
“…kumekuwa na matukio mbalimbali ya kikatili na mauaji ya watu wenye Ualbino nchini hivyo tunatumia nafasi hii kulaani vikali vitendo hivi visivyo na utu na vinavyokiuka haki za msingi za walemavu hao nakusababisha mateso makubwa hivyo sheria ziimalishwe kwa kuendesha kampeni za kuelimisha jamii iweze kuondokana na dhana potofu,”amesema
Naye Mkurungenzi Mtendaji wa Shirika la haki za Kisheria,maendeleo ya jamii na Uchumi(DOLASED),Wakili Gidion Mandes ameomba waajiri sekta binafsi na umma kuzingatia sheria na kanuni zilizopo ilikutoa fursa za ajira na kazi kwa watu wenye Ulemavu.
“Mbali na ajira tunaomba taasisi za fedha na mikopo kuwapa kipaumbele watu wenye Ulemavu iliwaweze kujiajiri na kuondoa utegemezi,kwani jamii imekuwa ukitumia fimbo ya Ulemavu kunyima nafasi kwa watu wenye changamoto hiyo nitoe rai kwa jamii ituamini kwani Ulemavu siyokutokujiweza,”Amesema
Maadhimisho hayo yamefanyika leo yakiwa na kauli mbiu ya “Kuongeza Uongozi wa Watu wenye Ulemavu kwa Mustakabali Jumuishi na Endelevu “