Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Bohari ya Dawa (MSD) Dkt. Rukia Mwifunyi amepongeza Kanda ya MSD Tanga kwa kuvuka malengo ya mauzo, katika robo mwaka ya kwanza ya mwaka kwa asilimia 12.
Mjumbe huyo wa Bodi, ambaye ni mlezi wa Kanda ya MSD TANGA amefuatana na Meneja Huduma za Sheria MSD, Elisamehe Macha katika ziara ya kutembelea wateja wanaohudumiwa na Kanda ya Tanga,ziara ambayo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka thelathini (30) ya utendaji wa MSD tangu kuundwa kwake.
Akizungumza na watumishi wa Kanda ya Tanga Dkt. Mwifunyi amemwelekeza Meneja wa MSD Kanda ya Tanga, Sitti Abdurahman kuhakikisha wanafuatilia kwa karibu madeni wanayowadai wateja wao.
Ziara hiyo inaendelea leo kwa kutembelea Hospitali ya Mkoa Bombo, na kituo cha afya Nkumba kilichopo Wilaya ya Muheza, mkoani hapa.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEggcjfnNgDBC0zcPNRYf8FgSvHvBVgl9L4VINg3VQpWkcqTPhHv9uuWL83wQL9lc0eorvxjgTGTJPoVfdA9I9DLKbTS1ghqIey7-CjHJVyxUsxr5057ttvGvTnrwIZFa-XvtOwh7MUNcKnlcUsmWfK25tij3s_uDXTgQgzc25uV7X6bDTozOJFQaiAPDOU/w640-h454/1%20MSD.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhqh2vTFo30bnVz5UUFonAFpUKOxJbO1sMjZ7ul0tFCj1RrWdRTYez5pRh4Bi2ft3znK6-xhyphenhyphen-EzzVxvfee5Q3x9WunUNVtnQ_AXkgtMyAqeXMxDuwUsJXfBExv4K00e8FbyKaahUjA1mGByO4C9A0yt4KEtR-lUmvQx6XPjAHARpP7YBYTVMHavXJ2UN0/w640-h292/2MSD.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiRbq1T6pCEpGNtzlMIH9uuvyGnFqXCGU5sqdgzExcRtMAKjKp_IQL1AI2rSq6ibkryagY_2QlLOJAZrDY7DLRUtnKVZhiVy3OE2dQnBTkDantG7Mbtxc8e-7zGxkdOu2qNJqmKAovBqJkRLsnjm776b35Cqpvwy4lHG_bNrLAVW_66N2Z8M5M9zbyCRLo/w640-h434/3.jpg)
Ziara hiyo ikiendelea
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiX0XFyAi8_ns_IocNl5c4AECg_PsdDzKWwjZE23DfqSO4zib9_HqMWX2-l5OzGGmrPOmpBul8rIXU4zkYqsRlRNnCy6iq4Du9AYrpTBr5vdWWFU_4pFRFaKrqveFSbqX5WCVUosqDpJPE15OIA7mJFFv_tlPfSJxtxRL9PlOt8ybNLtAjQWHXFLj3AvhI/w640-h400/6.jpg)
Muonekano wa uhifadhi wa bidhaa za afya katika Ghara la MSD Kanda ya Tanga
Magari ya MSD yanayotoa huduma ya kusambaza bidhaa za afya Kanda ya Tanga,
Muonekano wa Ofisi ya MSD Kanda ya Tanga
Meneja wa Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Tanga Sitti Abdulrahman (mbele) akiongoza msafara wakati wa kuelekea kutembelea Ghara za MSD wakati wa ziara hiyo. |
Utembeleaji wa Ghara hilo ukiendelea |
Watumishi wa MSD Kanda ya Tanga wakiwa katika picha ya pamoja na wa Bodi ya Udhamini ya MSD, wakati wa ziara ya kutembelea wateja wanaohudumiwa na Kanda ya Tanga Desemba 2, 2024.
PICHA ZOTE NA MTANDAO WA SINGIDANI BLOG-TANGA